Habari za Punde

Yanga, Mafunzo waingiza 5.5 m/-

KIASI cha shilingi 6,500,000, zimeingia kutokana na mapato ya milangoni, katika mechi mbili za kwanza za michuano ya Kombe la Mapinduzi juzi.

Mshika Fedha wa kamati ya mashindano hayo Amani Ibrahim Makungu, ameviambia vyombo vya habari kuwa, pambano la mchana kati ya Azam FC na Kikwajuni, liliingiza shilingi 1,050,000, wakati lile la usiku
lililozikutanisha Yanga na Mafunzo, lilivuna shilingi 5,450,000 taslim.

Makungu ameeleza matumaini ya kamati yake kuzidi viwango hivyo, kadiri mashindano hayo yatakapokuwa yakiendelea, akitarajiwa kuwa mechi ya jana kati ya Simba na Jamhuri, ingeweza kuvutia mashabiki wengi zaidi uwanjani.

Simba ina mashabiki wengi sana hapa Zanzibar, sawa na Jamhuri ambayo inapokutana na timu kubwa za Dar es Salaam, wapenzi wake kutoka kila pembe ya nchi hujitokeza na kuungana kuishangiria.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.