Habari za Punde

Miembeni Utd Yaizamisha KMKM

Na Hadia Khamis

TIMU ya Miembeni United, imefanikiwa kuwazamisha mabaharia wa KMKM kwa kuwafunga bao 1-0, katika mchezo wa kwanza kwa timu hizo kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi.

Mchezo wa kundi A ulichezwa wakati wa saa 10:00 jana jioni, ambapo washindi walipata bao lao kupitia kwa Issa Othman katika dakika ya 36.


Hata hivyo, pambano hilo lilikosa msisimko kwani washambuliaji wa timu zote walishindwa kufanya mashambulizi ya maana milangoni.

Makocha wa timu hizo, Said Kwimbi wa Miembeni United na Ali Bushiri wa KMKM, walilalamikia hali mbaya ya uwanja kuwa ndiyo iliyoufanya mtanange huo ukose mvuto.

Katika mfululizo wa ngarambe hizo, leo jioni Mafunzo itakwaruzana na Azam FC, wakati majeruhi Yanga, watajaribu kusaka ushindi wa kwanza mbele ya Kikwajuni wakati wa usiku.

Mchezo kati ya Azam na Yanga, unaotabiriwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na Yanga kufungwa na Azam 2-0 katika mechi ya kirafiki zaidi ya wiki moja iliyopita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.