Habari za Punde

Iran Kusaidia Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Zanzibar

Na Fatma Mzee-Maelezo 

Jumla ya Dola Milioni Tano zimetengwa na Serikali ya Iran kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Chuo cha Ufundi Zanzibar ikiwa ni hatua ya kwanza ya ujenzi huo.

Yameelezwa hayo na Mshauri wa Rais wa Mambo ya Utamaduni Nchini Iran Bw Sher Salahi huko Wizara ya Elimu alipokuwa akizungumza na Waziri wa Elimu wa Zanzibar Ramadhan Abdalla Shaaban huko Afisini kwake,


Amesema yeye pamoja na Ujumbe aliofuatana nao wamekuja kufuatilia makubalianao yao na kuona eneo ambalo limeshatengwa kwa ajili ya kazi hiyo kwa vile wako tayari kuanza kazi hiyo ya ujenzi

Naye Waziri wa elimu alieza kuwa kiwanja hicho ambacho kipo eneo la Tunguu bado kina malengo yale yale yalio kusudiwa hivyo kama Serikali ya Iran iko tayari ni vyema kuja kuanza ujenzi huo.

Amesema kuwa hiyo ni nafasi nzuri kwa Zanzibar kwani mbali ya kutoa taaluma itaweza kutoa ajira kwa vijana.

Aidha Waziri aliushauri ujumbe huo kuunda kamati amabayo itakuwa na kazi ya kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa mradi huo.

Mapema ujumbe huo ulipata nafasi ya kutembelea Afisi ya Nyaraka iliyopo Kilimani Mjini Zanzibar na kuweza kujionea jinsi nyaraka hizo zinavyo hifadhiwa

Chuo hicho kitakapomalizika kujengwa kinatarajiwa kusomesha mambo ya kuhifadhi Nyaraka kwa lengo la kuwa na Walimu na Wafanya kazi wenye uwezo wa kisasa wa kuhifadhi Nyaraka na kuweka kumbu kumbu kwa utaalamu zaidi.


IMETOLEWA NA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.