Na Suleiman Rashid Omar, Pemba
WANANCHI wa Mtambwe Nyali katika wilaya ya Wete wamepongezwa kwa jitihada kubwa walizozichukua za kuunda vikundi vya ushirika vya uzalishaji mali ambavyo vimekuwa msaada mkubwa kwenye mapambano dhidi ya umasikini.
Mbunge wa jimbo hilo, Dk. Said Suleiman Said, alieleza hayo kwenye ziara ya kutembelea miradi mbali mbali ya vikundi vya ushirika vikiwemo vya ufugaji wa samaki, kaa pamoja na upandaji wa miti.
Alisema kufanyakazi kwa pamoja katika vikundi vya ushirika ndiyo ufumbuzi wa utatuzi kero ya kuondosha umasikini katika jamii na kuzipongeza jitihada za wananchi hao kwa kuanzisha vikundi hivyo.
Mbunge huyo alifahamisha kuwa suala la upandaji miti katika fukwe na ukulima wa mazao ya biashara kama vile minanasi yataleta mabadiliko ya haraka ya kiuchumi katika maisha ya wananchi hao.
Alisema ili kuyafanya maeneo mbali ya vijiji hasa vilivyoko kando ya bahari kuwa na maisha bora naendelevu ni wakaazi kuitunza kwa kujihimiza kupanda miti maeneo ambamo yame kufa kama wanacvyo fanya
wananchi hao wa mtambwe.
Aliahidi kuwapatia mabwela suti ya kufanyia kazi na viatu vya ‘rainboot’ vikundi viwili vya ufugaji wa samaki na pia kuwapatia pampu ya kutolea na kuingizia maji kikundi cha kufugia samaki kilichopo kwa Gando,
Nyali na Mtambwe.
Wakizungumza katika ziara hio katibu wa kikundi cha ufugaji samaki kilichopo kwa Cheusi Nyali, Bakari Sharifu alisema juhudi zao tayari zimeanza kuzaa matunda kwani samaki zaidi ya 1000 wapo karibu kuvuna
huku vifaranga walio ingiza hivi karibuni ni zaidi ya 1500.
Alisema kuwa vitendea kazi na taluma ya kutosha katika shughuli zao ni tatizo linalo wakwaza hadi sasa kwa vile kila wanapo hitaji fedha hulazimika kupiga mchango kwa kila mwana ushirika huku ufugaji wenyewe
ukuinda kwa mazoea hakuna.
No comments:
Post a Comment