Na Farida Abdallah MUM
BAADHI ya wafanyabiashara wa soko la Darajani wameilalamikia Baraza la Manispaa kuwatoza kiwango kikubwa cha fedha kwa ajili ya leseni ya biashara ambayo hailingani na biashara wanazozifanya sokoni hapo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao walisema wamekuwa wakitozwa kiwango kikubwa cha fedha kwa ajili ya leseni kwa mwaka pamoja na ushuru wa kila siku fedha ambazo haziendani na biashara zao.
Yussra Mohammed mfanyabiashara wa chai na vitafunio sokoni hapo aliliambia gazeti hili kuwa lengo la kujiajiri ni kupambana na umaskini uliokithiri lakini kitendo cha Baraza la Manispaa kuwatoza fedha nyingi hakiwasaidiii kufanikisha malengo yao zaidi ya kuwaongezea hali ngumu ya maisha.
Alisema" mtaji wa biashara yangu hauzidi elfu ishirini, leseni kwa mwaka ni elfu hamsini achia mbali ushuru wa kila siku wa shilingi mia tano uuze ama usiuze....."
Nae mfanyabishara wa mboga mboga Bakari Alli Mussa alisema pamoja na kutozwa viwango vikubwa vya fedha za leseni na ushuru' bado hali ya soko hilo hairidhishi kwani baadhi ya mabanda ya biashara yapo katika
hali mbaya hasa katika msimu huu wa mvua kwani mengi yao yanavujisha maji hivyo hupelekea bidhaa zao kuharibika.
Mfanyabiashara huyo alishauri kuwa fedha ambazo wanalipa kila siku na kila mwaka zitumike katika kuwatengenezea mazingira mazuri ilikuongeza tija katika baishara zao.
Aidha kwa upande wa baraza la Manispaa chini ya mkuu wa Mapato Bidaya Masoud alisema kuwa kiwango cha fedha cha elfu hamsini kwa ajili ya malipo ya leseni ni kidogo ukilinganisha na matumizi ya soko hilo na ni wazi kuwa hakikidhi haja ya maendeleo ya sokoni hapo.
Bidaya aliwataka wafanyabiashara waache kulalamika kuhusu viwango hivyo kwani vimekuwa kwa manufaa yao wenyewe, mfano ushuru wa shilingi mia tano kila siku ni kwa ajili ya usafi wa sokoni hapo na leseni ni
kwa ajili ya maendeleo ya soko hivyo waandelee kushirikana na serikali katika kuchangia mapato hayo.
No comments:
Post a Comment