Na Mwanajuma Mmamga
HAKI ya kumlinda na kumpa matunzo mototo ni ya kila mmoja katika jamii na sio jukumu la baadhi ya watu na taasisi fulani.
Daktari katika kituo cha ‘One stop Center’, kiliopo Mnazimmoja, Salum Omar Mbarouk alieleza hayo alipokuwa akiwasilisha mada juu ya matunzo kwa watoto yaliyofanyika katika kituo cha walimu (TC), Mkwajuni mkoa wa Kaskazini Unguja.
Alisema katika uhifadhi na ulindaji wa watoto katika mkoa huo uwe mfano bora na kuleta mashirikiano ya pamoja katika vijiji jirani.
Alifahamisha kuwa kuwepo kwa ushirikiano kutaleta ufanisi mkubwa katika suala zima la kumlinda na kumuhifadhi mtoto hasa ikizingatiwa kuwa jukumu hilo ni la jamii nzima.
Akifafanua kuhusu ushirikiano wa kumuhifadhi mtoto Ofisa hifadhi ya mtoto, Mkasi Abdalla Rajab amesema Idara ya Ustawi wa Jamii haiwezi kumuhifadhi mtoto pekee bila kushirikiana na vyombo vyengine kama
habari, polisi, mahakama na ofisi ya Muendesha Mashtaka.
Nae Mwanasheria wa Idara ya Chuo cha Mafunzo, Seif Maabad Makungu alisema yapo makundi hatarishi ya watoto yanayosababishwa ugumu wamawasiliano, kutengwa, utashi wa wazazi, kukosa mahitaji ya
kutofahamika hatari na viashiria vya hatari.
Akitoa mfano makundi hayo alisema ni pamoja na watoto wenye ulemavu na watoto wa mitaani waliokosa makaazi.
No comments:
Post a Comment