Na Madina Issa
MWENYEKITI wa jumuia ya ‘Zanzibar Outreach Program’ (ZOP), Walid Kassim Muhammed amewataka wananchi katika maeneo mbali mbali kujitokeza kwenda kupatiwa matibabu pale wanaposikia inakwenda kutoa matibabu vipimo.
Mwenyekiti huyo alieleza hayo hivi karibuni huko Matemwe mkoa wa Kaskazini Unguja, ambapo watalamu wa afya wa ZOP walifika kuwafanyia vipimo wananchi pamoja na kutoa matibabu.
Alisema wananchi hao watapofika kuonana na watalamu wa ZOP katika maeneo wanayofika, wataweza kupimwa pamoja na kupatiwa matibabu ya magonjwa yanayowasumbua.
“Tunapotoa matangazo ya kufika sehemu fulani kwa ajili ya kupima na kutoa matibabu wananchi fikeni kwa wingi, huduma hizi ni kwa ajili yenu”,alisema Mwenyekiti huyo.
Alisema mbali ya kufanya vipimo na kutibu matatizo kama vile ya macho, koo, masikio na shindikizo la damu, pia wataalamu wa ZOP wamekuwa wakitoa ushauri ambao kama utafuatwa huasaidia wananchi kuepuka
maradhi mbali mbali.
Nae Dk. Muhidin Mohammed, alieleza kufurahishwa na wanakijiji wa Matemwe kwa kuitikia wito wa kushiriki kwenye kambi ya matibabu.
Hata hivyo aliwataka wananchi wengine waliokuwa hawajijitokeza katika huduma hiyo maondoshe dhana kwa huduma inayotolewa na madaktari hao kwani madaktari hao ni wazuri na waliosomea na wala wawajifundishi kupitia kambi za ZOP.
Hata hivyo aliwataka madaktari wengine kujitokeza kwa wingi kutoa huduma kwa wananchi wa vijijini kwa moyo wao ili waweze kuwasaidia kuwatatulia matatizo yao yanayowakabili siku hadi siku ambayo hawayajui.
Nao wanakijiji hao wamewapongeza madaktari wa jumuiya hiyo kwa kuwapelekea huduma hiyo kijijini kwao kwani yamekuwa adimu kwa wanakijiji hao na kwa hivi sasa wameweza kugundua matatizo yanayowakabili siku hadi siku.
No comments:
Post a Comment