Na Boniphace Makene, DAR
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal jana amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi wapya wa nchi za Saudia, Uturuki na Vatican ambao walifika ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Balozi wa Saudi Arabia, Hani Abdullah Mo’minah, alisema nchi yake itahakikisha inakuza uhusiano wa kibishara baina yake na Tanzania.
Alisema chini ya mpango huo Balozi huyo alimueleza Dk. Bilal kuwa inaandaliwa mipango ya kuwakutanisha wafanyabiashara wa Saudi Arabia na wenzao wa Tanzania katika kubadilishana ujuzi na kutanua nafasi zao za kuwekeza katika nchi hizi mbili.
Aidha Balozi Mo’minah alizungumzia juhudi za nchi yake kuhakikisha inakuwa na makazi ya kudumu nchini Tanzania, jambo ambalo litawapunguzia gharama za uendeshaji ofisi yao katika jiji la Dar es Salaam.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais Dk. Bilal alimueleza Balozi huyo kuwa Tanzania ina uhusiano mzuri na Saudi Arabia na lengo ni kudumisha uhusiano huo, na kueleza kuwa atafurahia kuona wafanyabiashara wa nchi hizi mbili wanakutana na kubadilishana uzoefu ili kukuza sekta hiyo kwa faida ya nchi hizo.
Naye Balozi wa Uturuki nchini, Ali Davutoglu alisema kuwa nchi yake ipo tayari kuwekeza katika ujenzi wa Chuo Kikuu ili kukuza sekta ya elimu nchini hali inayotokana na skuli kadhaa zinazomilikiwa na Waturuki zilizo katika viwango vya skuli za Awali, Msingi na Sekondari kuonekana kufanya vema katika mitihani ya kitaifa.
Balozi huyo alisema kutafanyika kongamano la wafanyabiashara wa Tanzania na Uturuki katika mwezi Mei mwaka huu, na kwamba kongamano hilo lina lengo la kuonesha fursa za kiuchumi zilizopo katika nchi hizo.
Dk. Bilal alimuelezea Balozi Davutoglu kuwa, uwekezaji katika elimu sasa

No comments:
Post a Comment