Habari za Punde

Kikosi cha Zima Moto chafanikiwa kuzima Moto katika Jengo la ZSSFKilimani.

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, asalimiana na Kamanda wa Kikosi cha Zima moto alipowasili katika Viwanja vya Jengo la ZSSF Kilimani kuangalia tukio la moto lilotokea katika gorofa yake ya nne katika moja chumba cha jengo hilo, katika ajali hiyo hakuna mtu aliyejeruhiwa. 
 Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, Khamis Filifili, akitowa maelezo kwa Makamu wa Pili w Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, alipotembela jengo hilo kuangalia athari ya moto huo, uliosababishwa na hitilafu ya umeme katika moja ya chumba katika jengo hilo.    
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, akiagalia chumba kilichotokea moto huo katika jengo la ZSSF Kilimani, katika moto huo hakuwa mtu aliyejeruhiwa wala uharibufu mkibwa wa mali.  
 Hiki ndicho chumba kilichotokea hitilafu ya umeme na kuwaka moto katika jengo la ZSSF Kilimani leo asubuhi.
 Jengo la ZSSF Kilimani, ambalo moja ya chumba chake kiliwaka moto uliotokana na hitilafu ya umeme katika chumba hicho kilioko gorofa ya nne,ambako kulikuwa kumekondishwa na Bodi ya Mapata Zanzibar ZRB. Wananchi wakiwa nje ya Jengo la ZSSF Kilimani wakiangalia moto ukiwaka katika jengo hilo katika moja ya Vyumba vya jengo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.