Habari za Punde

Skuli ya International Yatamba Judo.

Na Asya Hassan

IBRAHM Mohammed kutoka Amani, amefanikiwa kushinda mkanda kijani baada ya kushinda mchezo wa judo katika mashindano yaliyoshirikisha wanafunzi wa skuli ya International ya Mazizini na watoto wa Amani na Mlandege.

Mashindano hayo yaliyofanyika katika skuli hiyo, yalijumuisha wachezaji watoto12 ambapo kabla ushindi wake huo, Mohammed alikuwa na mkanda mweupe na hivyo kupiga hatua moja zaidi.


Washiriki wengine waliokwaa mkanda wa kijani, ni Abdulshakur na Miron Stritter ambao awali walikuwa na mikanda wa njano, huku Salum Nasri Said na Suleiman Hamad wakivaa mkanda wa njano pia.

Akizungumza baada ya mashindano hayo, Mwalimu Mkuu wa skuli hiyo Terry Binns, alisema lengo la michuano hiyo ni kumuenzi aliyekuwa mwalimu wa mchezo huo Abubakar Saleh Mohammed aliyefariki mwezi Januari mwaka huu, ambaye alikuwa akifundisha mchezo huo skulini hapo.

Naye Rais wa Chama cha Judo Zanzibar (ZJA) Tsuyoshi Shimaoka, aliwataka walimu kuwaendeleza watoto ili wapate ufanisi katika mchezo huo, kwani michezo ni njia muafaka ya kuitangaza Zanzibar nje ya nchi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.