Habari za Punde

Taarifa ya Mhe. Hamad Masoud Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu kwa Waandishi wa Habari

TAREHE 27 MACHI, 2012

UTANGULIZI:

Ndugu Waandishi wa habari, sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha tena kwa mara nyengine tena, mimi binafsi na watendaji wote wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano tunapata faraja kubwa kuwa nanyi hii leo katika kueleza utekelezaji wa majukumu yetu ya kila siku.

Ndugu waandishi wa habari, kama mnavyojua Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano imegawika katika sehemu kuu zifuatazo:-

1. Idara ya Mipango, Sera na Utafiti

2. Idara ya Utumishi na Uendeshaji

3. Idara ya Mawasiliano

4. Idara ya Usafiri na Leseni

5. Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara

6. Mamlaka ya Viwanja vya Ndege

7. Mamlaka ya Usafiri wa Baharini

8. Shirika la Banadari

9. Shirika la Meli

10. Ofisa Mdhamini – Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano – Pemba

Ndugu Waandishi wa habari, katika utekelezaji war obo mbili hizi (yaani kuanzia Julai – Septemba na Oktoba – Disemba 2012) kuna mafanikio kadhaa yaliyopatikana kupitia Idara zetu ambayo nitayaeleza kwa kila Idara pamoja na chamgamoto na matarajio ya baadae.

DARA YA MIPANGO SERA NA UTAFITI

1.0 KAZI ZA IDARA

i. Kupanga, kuratibu, kusimamia na kutathmini utekelezaji wa sera na mipango ya sekta ndogo za usafiri wa baharini, nchikavu na anga na teknolojia ya habari na mawasiliano.

ii. Kuratibu kazi zote za maendeleo za Wizara zikiwemo kubuni, kutayarisha na kusimamia na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo;

iii. Kufanya tafiti mbalimbali za maendeleo katika sekta ya miundombinu na mawasiliano;

iv. Kukusanya, kuchambua na kuwasilisha takwimu zinazohusiana na sekta ya usafiri na mawasiliano;

v. Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli za mpango mkakati, bajeti, MTEF, MKUZA , na masuala mtambuka ya ukimwi na jinsia, na kuratibu kazi za taasisi za Muungano zinazohusu sekta ya miundombinu.

2. MALENGO YA IDARA

Ndugu waandishi wa habari, Kwa mwaka wa 2011/2012, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti ina malengo yafuatayo:

i. Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Usafiri, na Mpango Mkuu wa Usafiri wa Zanzibar (Zanzibar Transport Masterplan),

ii. Kukamilisha taratibu za uanzishwaji wa Mamlaka ya Kusimamia Usafiri wa Baharini Zanzibar (Zanzibar Maritime Authority),

iii. Kuandaa sheria ya uanzishwaji wa Mamlaka ya Barabara.

iv. Kusimamia miradi yote ya Wizara,

v. Kutayarisha sheria na kanuni mbali mbali za udhibiti wa sekta ndogo za usafiri.

vi. (vi) Kuandaa sera ya teknolojia ya habari na mawasiliano ili iweze kuongoza maendeleo ya sekta hiyo kwa lengo la kuingiza Zanzibar katika matumizi ya teknolojia ya habari;

vii. Kuendelea kuratibu shughuli zote za mipango, sera na utafii za Wizara,

MAFANIKIO YA IDARA

Katika kipindi mwezi Disemba 2011 hadi Machi 2012 Idara imepata mafanikio yafuatayo:

i. Imeendelea kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkuu wa Usafiri wa Zanzibar ambapo imefanikisha kupatikana kwa fedha kwa ajili ya awamu ya pili na tatu ya marekebisho ya muundo wa kitaasisi wa Wizara;

ii. Imeratibu ukamilishaji wa rasimu ya Sheria ya uanzishwaji wa mamlaka ya barabara na rasimu ya Sheria ys Shirika la Meli la Zanzibar

iii. Imeendelea kuratibu taratibu za uanzishwaji wa Mamlaka ya Kusimamia Usafiri wa Baharini Zanzibar (Zanzibar Maritime Authority),
Imeendelea kuratibu hatua za utayarishaji wa sera ya teknolojia ya habari na mawasiliano.

v. Imeratibu kuundwa kwa Kamati za kuanzisha Chuo cha Mabaharia na Chuo cha Marubani Zanzibar;

vi. Imekamilisha maanadalizi ya mchakato wa kuandaa Bajeti ya Wizara ya Mwaka 2012/13 inayojumuisha utayarishaji wa bajeti kwa njia ya program (program based budget ) na MTEF.

vii. Imekusanya takwimu za sekta ya usafiri na mawasiliano kwa kipindi hicho cha miezi mitatu;

iii. Imesimamia kukamilika kwa utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Vijijini Kusini Pemba, Mradi wa Barabara ya Amani-Dunga, na Mradi wa Barabara ya Bumbwini.

ix. Imeendelea kusimamia Mradi wa Ujenzi wa Barabara Tatu za Pemba (kilomita 52.7), Mradi wa Ujenzi wa Barabara za Vijijini za Kaskazini Pemba MCC (kilomita 43.8); Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Abiria la Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume,Unguja.

x. Imeendelea kuratibu uchunguzi wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara zinazoingia Mjini (Urban Entry Roads ) na Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya MpigaDuri ( Hub Port Project);
Imeendelea kuratibu mchakato wa kutafuta taratibu za utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Ole-Kengeja.

xii. Imeendelea kuratibu mahudhurio ya viongozi, watendaji na wataalamu wa Wizara katika vikao, semina na warsha za kitaifa, kikanda na kimataifa.

xiii. Imeendelea kutayarisha ripoti na nyaraka mbali mbali zinazokwende ndani na nje ya nchi;

xiv. Imeendelea kuratibu masuala mtambuka ya Ukimwi, Jinsia, na Mazingira katika Wizara.

4.0 CHANGAMOTO

Idara imekuwa ikikabiliwa na changamoto zifuatazo:

i. Ufinyu wa bajeti na kutoingiziwa fedha kwa wakati kunaathiri utendaji wa kazi za Idara;

ii. Uhaba wa wataalamu katika fani mbali mbali ;

iii. Kutokuwepo jengo la kudumu la Wizara ;

iv. Ukosefu wa vitendea kazi.

4.1 Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali. Wataalamu mbali mbali wataendelea kutafutwa na wengine kupatiwa mafunzo. Vitendea kazi vitaimarishwa na Wizara itaendelea na juhudi za kujenga jengo jipya la kudumu la Wizara.

IDARA YA UTUMISHI NA UENDESHAJI

Idara ya Uendeshaji na Utumishi ni moja kati ya idara tisa za Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano. Idara hii inasimimamia kazi zifuatazo-:

• Kushughulikia kazi za uendeshaji za kila siku katika Wizara

• Kushughulikia maslahi ya wafanyakazi wa Wizara

• Kusimamia nidhamu za wafanyakazi wa Wizara

• Kushughulikia mpango wa mafunzo kwa wafanyakazi wa Wizara

• Kusimamia mpango wa elimishaji wa masuala ya ukimwi

1. KAZI ZA UENDESHAJI

Idara imekuwa ikisimamia utekelezaji wa kazi zake za kila siku za uendeshaji wa ofisi kwa kuhakishia kuwa vitendea kazi vyote vinapatikana bila ya usumbufu wowote na kuhakisha kuwa wafanyakazi wanaendelea kufanya kazi katika mazingira mazuri na ya kuridhisha aidha idara imeendelea kuratibu shughuli za utendaji kazi kwa viongozi wa wizara na watendaji wengine na kusimamia ziara zao za ndani ya nchi na nje ya nchi.

Idara kwa kushirikiana na Wizara ya Utumishi wa Umma inaendelea na kazi ya kutayarisha muundo wa utumishi wa Wizara ilikuhakisha kuwa wafanyakzi wanapangiwa majukumu yao ya kazi kwa mujibu wa elimu zao “Job Description”

Idara imeendelea kusimamia kazi za utunzaji wa kumbukumbu za wafanyakazi na za Wizara kwa ujumla. Kitengo cha Nyaraka “Documentation” kimeimarishwa zaidi na kuboreshwa na kuweza kumudu kuzitunza vyema nyaraka na mikataba yote ya Wizara na kumbukumbu nyingine ambazo ni muhimu kwa ajili ya matumizi ya sasa na ya baadae.

2. MASLAHI YA WANYAKAZI

Wafanyakazi wote wa wizara wamekuwa wakipatiwa maslahi yao kwa mujibu wa stahiki zao ikiwemo malipo ya mishahara, likizo na malipo ya baada ya saa za kazi. Jumla ya wafanyakazi 25 wamekwenda likizo zao na kulipwa mafao yao.

kuwa fedha hizo zinarudishwa benki kwa mujibu wa taratibu zilizokubalika na benki. Jumla ya wafanyakazi 36 wamestaafu na wamepatiwa stahiki zao kwa mujibu wa sheria za utumishi serikalini.

3. MAFUNZO

Idara imekuwa ikiendelea kusimamia mafunzo wafanyakazi wa Wizara kwa kuhakisha kuwa wanapatiwa mafunzo ya muda mfupi na muda mrefu ya ndani na nje ya nchi.

IDARA YA MAWASILIANO

Idara hii ni miongoni mwa Idara tisa zinazofanya kazi ndani ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.
Majukumu makuu ya Idara hii ni kuratibu na kusimamia mambo yote yanayohusiana na huduma za mawasiliano katika visiwa vya Zanzibar.

 Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kupitia Idara hii inaendelea na juhudi zake za kuimarisha huduma bora za mawasiliano. Sekta hii ni muhimu na inayoendelea kukua kwa kasi kubwa hii inatokana na ulimwengu mzima kutilia mkazo katika sekta ya Sayansi na Tekonolojia.

 Zanzibar kama nchi nayo haiko nyuma inajitahidi kwenda na kasi hiyo huku ikielewa kuwa kuimarika kwa sekta hii ndio chachu ya Maendeleo ya Nchi yetu ikiwemo ustawi wa jamii na ukuaji wa Uchumi na pato la Taifa. Sekta Hii inajumuisha utoaji wa huduma za mawasiliano kwa njia ya Simu, Posta na huduma za teknolojia ya habari (IT).

 Idara inaaendelea kushirikiana na kampuni zinazotoa huduma za mawasiliano kwa kuendesha vikao vya pamoja kwa kuweka misingi ya mashirikiano baina ya taasisi hizo kwa lengo la kupata mafanikio kwa nia ya kuhakikisha kuwa Wananchi wa Zanzibar wanapata huduma bora, salama na endelevu ambazo zitawezesha kukuza kipato kwa Mwananchi mmoja mmoja na uchumi wa Taifa kwa ujumla kwa kupitia Sekta ya Mawasiliano.

 Sekta ya mawasiliano hapa kwetu imekuwa ikiipa changamoto idara yetu ya kusimamia utendaji wa kazi hizo, kama tunavyofahamu washiriki wakubwa wa sekta hii ni taasisi binafsi, ambazo ndizo zilizojiimarisha katika utoaji wa huduma za mawasiliano. Taasisi za umma zinazojishughulisha na kazi hii bado ni chache sana.

 Idara ya Mawasiliano kupitia kamati ya ukaguzi na ujenzi wa Minara, imekuwa ikiratib ujenzi wa minara ya Mawasiliano na simu kwa kutoa vibali kwa makampuni yanayohitaji kujenga minara hiyo. Kamati hufanya ukaguzi na iwapo imeridhika kuwa eneo hilo lipo salama na linafaa kwa ujenzi mnara unayojengwa na makampuni husika hutoa kibali cha ujenzi huo kwa Unguja na Pemba. Kamati ya ukaguzi na ujenzi wa Minara imehusisha taasisi nyingine za Serikali ikiwemo Mazingira, Ardhi, Tawala za Mikoa na Mawasiliano.

 Kwa mwaka 2011-12 kamati imeweza kufanya ukaguzi na kuruhusu ujenzi wa minara mipya 25 kati ya 28 iliyoombwa kujengwa.

 Kamati inajitahidi kufanya kazi ili kuhakisha kuwa huduma zilizo bora katika maeneo yote ya Zanzibar zinapatikana na kupunguza malalamiko kati ya watoa huduma na watumia huduma za Mawasiliano kwa Unguja na Pemba.

 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inamiliki mnara Wireless ambao ni mnara mkongwe na mkubwa kuliko yote iliyopo hapa Zanzibar. Mnara huu ulijengwa zaidi ya miaka 100 iliyopita na ulitumika kwa kutoa huduma za mawasiliano yote kwa nchi zote zilizopo katika ukanda wa Afrika Mashariki, tokea kujengwa kwake hadi miaka ya 80 mnara huu ulikuwa unafanyiwa matengenezo ya mara kwa mara na Serikali, baada ya hapo Serikali ilishindwa kuufanyia matengenezo hayo kutokana na hali ya kifedha.

Ndugu waandishi wa habari,

Idara hivi sasa imo katika hatua za mwisho kukamilisha sera ya matumizi ya huduma za Teknologia ya habari na mawasiliano (Tehama) kwa Zanzibar.

Wizara ya Mawasiliano kwa kushikiana na Tume ya Utangazaji Zanzibar na wadau wengine tunaendelea na hatua ya kuratibu mabadiliko ya utengenezaji wa mfumo wa kiteknologia kutoka analogia kwenda Digitali ambayo yatalenga zaidi kwenye matumizi ya huduma za TV. Idara kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inaendelea na hatua za kitaifa za uanzishwaji wa anuani za simbo (Post Code) kama ilivyopangwa kwa Tanzania nzima.

CHANGAMOTO.

1. Uhaba wa vifaa na wataalamu waliobobea katika fani mbali mbali za mawasiliano ambazo kila siku zinakuwa kwa kasi zaidi,

2. Uhaba wa bajeti iliyopangiwa Idara imekuwa inashindwa kuhudhuria vikao tofauti vya kimataifa kwenye fani ya mawasiliano ambavyo dunia inakuwa na maazimio Fulani ya kutekelezwa kwa kila nchi hii inaifanya Zanzibar kuwa nyuma kila siku,

3. Maingiliano ya kazi za sekta ya Mawasiliano na taasisi nyingine za Serikali.

Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali.

IDARA YA USAFIRI NA LESENI

Idara ya Usafiri na Leseni ni moja kati ya taasisi iliopo chini ya Wizara Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar,Idara hii ndio msimamizi mkuu wa usafiri wa barabarani katika visiwa vya Unguja na Pemba.

KAZI ZA IDARA

Idara ya Usafiri na Leseni inatekeleza kazi zifuatazo:-

1. Kusimamia magari yanayotoa huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo.

2. Kusimamia utoaji wa leseni za kujifundishia na kuendesha vyombo vya moto

3. Kusimamia skuli za udereva pamoja na walimu wao.

4. Kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto vinavyotumia barabara.

5. Kuwafanyia majaribio ya nadharia na vitendo waombaji wa leseni za kuendesha vyombo vya moto vinavyotumia barabara.

6. Kuendesha na kusimamia Karakana Kuu ya Serikali ilioko Chumbuni na sehemu ya Mitambo ilioko Pemba.

MALENGO YA IDARA

Ndugu waandishi wa habari,

1. Kuhakikisha vyombo vyote vinavyotembea barabarani vimekaguliwa ili kuhakikisha uzima wake.

2. Kuchukua hatua mbalimbali kwa wale wanaovunja sheria za usafiri wa barabara.

3. Kuimarisha Karakana Kuu ya Serikali kwa kuipatia vifaa vya kisasa ili iende sambamba na mabadiliko ya technologia ya magari yanayoingia inchini.

4. Kuwapatia mafunzo watendaji wa Karakana Kuu ili wawe na ujuzi stahiki wa technologia ya magari ya kisasa.

5. kutengeneza vitambulisho kwa wanafuzi,walemavu na wazee wasiojiweza ili kuwawezesha kupata usafiri kwa nusu nauli.

6. kutoa muongozo juu ya wajibu wa makonda na madereva ili waweze kutoa huduma bora ya usafiri wa barabara.

UTEKELEZAJI WA KAZI

Katika kipindi cha disemba 2011 mpaka Februari 2012 Idara ya Usafiri na Leseni imetekeleza kazi zifuatazo:-

1. UTOAJI WA RUHUSA ZA NJIA: Katika kipindi hicho idara imetoa jumla ya ruhusa za njia 791 kwa vyombo mbali mbali vya biashara, kati ya vyombo hivyo 143 gari za mizigo, 268 daladala, 158 shamba, 181private hire,16 wanafunzi, na 25wafanyakazi.

2. UKAGUZI WA VYOMBO:Katika kipindi hicho jumla ya magari 7,877 yamekaguliwa kati ya vyombo hivyo 4,094 gari na 3,783 vyombo vingine.

3. UPASISHAJI WA MADEREVA:Jumla ya madereva 1,529 wamefanyiwa mitihani ya nadharia na vitendo, kati ya madereva hao 854 gari na 675 vyombo vya maringi mawili.

4. UTOAJI WA LEARNERS:Jumla ya lena 2,204 zimetolewa kwa wanafunzi wa ngazi mbalimbali wanaojifundisha kuendesha vyombo kati ya lena hizo 858 daraja A,12 B,817 B1,52 C,113 C1,91 D,233 D1,na 28 daraja M.

5. UKUSANYAJI WA MAPATO.Katika kipindi hicho Idara ya Usafiri na Leseni imekusanya jumla ya Tsh/=78,018,500.

MAFANIKIO YA IDARA.

1. Kurahisisha usafiri kwa wananchi wa mjini na mashamba kwa kuongeza idadi ya njia kwenye maeneo yaishio wananchi.

2. Idara imeanza kusajili magari na vyombo vya maringi mawili vya serikali ili kujua idadi halisi ya magari yanayomilikiwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

3. Idara imeweza kuendesha “operations” 5 za ukaguzi wa magari na vyombo vitembeavyo barabarani.

4. Idara imeanza kutoa vibali kwa magari ya kukodisha wageni (watalii).

5. Idara imekamilisha mchakato wa uvaaji wa sare kwa makonda na madereva wa magari ya abiria ya mjini na mashamba.

CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI IDARA.

1. Upungufu mkubwa wa vitendea kazi.

2. Uchakavu wa vifaa na mitambo ya Karakana Kuu ya Serikali na sehemu ya mitambo Pemba.

3. Upungufu mkubwa wa mafundi katika Karakana Kuu ya Serikali iliopo Chumbuni na sehenu ya mitambo ilioko Pemba.

4. Ukosefu wa jengo la ukaguzi na vifaa vinavyohitajika kwa shughuli za ukaguzi wa magari.

5. Uchakavu wa jengo la Makao Makuu ya Idara Mwanakwerekwe.

6. Uvunjaji wa sheria za usafiri barabarani kwa makonda na madereva wa vyombo vya moto.

IDARA YA UJENZI NA UTUNZAJI BARABARA

Idara ya Ujenzi na Utunzaji wa Barabara (UUB) ni moja kati ya Taasisi ambayo iko chini ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano.

KAZI ZA IDARA ZA KILA SIKU

Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara inafanya kazi kama ivuatavyo;

a) Kujenga na kusimamia kazi za Ujenzi wa Barabara mpya.

b) Kusimamia na kutekeleza kazi za Utunzaji wa Barabara

c) Kufanyakazi za Matengenezo makubwa na madogo ya Mitambo na zana inayotumika katika matengenezo ya Barabara.

d) Kufanyakazi za kawaida za kiuawala na za Kiutumishi za Idara.

MALENGO YA IDARA

Ndugu waandishi wa habari,

Idara ya Ujenzi na Utunzaji Barabara ina malengo yafuatayo;

a) Ujenzi wa Miundombinu bora na endelevu kwa ajili ya kushajihisha maendeleo ya kiuchumu na kijamii

b) Kuzitunza na kuzifanyia matengenezo stahiki barabara za Unguja na Pemba ili ziweze kupitika wakati wowote.

MAFANIKIO:

Idara imefanikiwa kujenga barabara nyingi Vijijini za lami na za kifusi Unguja na Pemba hivyo kupelekea yafuatayo;

a) Kupunguza usumbufu wa usafiri kwa abiria na mizigo.

b) Kupunguza gharama za matengenezo ya magari.

c) Kuchochea ongezeko la huduma nyengine za Kijamii na za kiuchumi mfano; ujenzi wa makaazi ya watu, maskuli, Hospitali, Maduka pamoja na shughuli za kiutalii na kadhalika.

d) Kutoa ajira kwa vikundi jamii na Wakandarasi wazalendo katika kazi za matunzo ya barabara hivyo kuongeza ajira kwa Wananchi.

Idara pia imefanikiwa kuzifanyia matengenezo stahiki barabara za Mjini na kuzifanya huduma za usafiri kuimarika.

CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI IDARA

Utendaji wa Idara haufikii lengo linalokusudiwa kutokana na kukabiliwa na changamoto zifuatazo;

a) Upungufu na uchakavu wa zana na mitambo kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa barabara.

b) Gharama kubwa za vipuri (spare parts) pamoja na kuchelewa kupatikana kutokana na kutokuwepo maduka na vipuri hivyo hapa Zanzibar.

c) Uvamizi wa maeneo ya hifadhi ya barabara ambao hupelekea fidia kubwa wakati wa Ujenzi wa Barabara.

d) Upungufu wa Wataalamu katika fani ya Uhandisi na taaluma nyengine zinazohusiana na Ujenzi wa Barabara.

Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali.

MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE

1. KAZI ZA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE

Mamlaka ya Viwanja vya ndege inaratibu na kusimamia maendeleo ya usafiri wa anga Zanzibar pamoja na uendeshaji wa Viwanja vya ndege Unguja na Pemba.

Aidha majukumu ya Mamlaka ni kusimamia huduma za usafiri wa anga, kuimarisha usalama wa ndege, abiria na mizigo. Majukumu haya yanatekelezwa na Mamlaka ya Viwanja vya ndege Zanzibar, kwa mashirikiano ya pamoja na taasisi mbali mbali za Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na secta binafsi.

 MALENGO YA MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE

Ndugu waandishi wa habari,

i. Ujenzi wa Uzio

- Ujenzi wa uzio kuzunguuka uwanja wa ndege wa (AAKIA) yenye jumla ya kilomita 12, kwa kumaliza nusu ya mwisho ya uzio, hadi sasa eneo la kilomita 1.1km, tayari limesafishwa.

ii. Ujenzi wa jengo jipya la abiria (terminal building)

iii. Ujenzi wa maegesho na njia ya kupitia ndege (extension of apron and taxiway)

iv. Uimarishaji wa huduma za Viwanja vya ndege.

v. Ukusanyaji wa mapato.

. MAFANIKIO YALIYOFIKIWA.

4. TAARIFA ZA UTEKELEZAJI:

NAM. KAZI HATUA ILIYOFIKIWA

1. Ujenzi wa uzio kuzunguka Uwanja wa ndege AAKIA wenye jumla ya (km 12)

Kumaliza nusu ya mwisho ya uzio Eneo la kilomita 1.1 tayari limesafishwa mita 246 zimeshachimbiwa mashimo na nguzo 84 zimewekwa

2. Mradi wa Ujenzi wa Jengo jipya la Abiria la Uwanja wa ndege (AAKIA)

i) Ujenzi wa Jengo la mitambo/abiria:

- Ujenzi wa msingi na nguzo la chuma kwa jengo la abiria

- Ujenzi wa jengo la mitambo

- Ujenzi wa tangi la maji

- Uwekaji wa paa la jengo

- Uwekaji wa kuta la vioo kwa jengo la abiria

Umemalizika

Unaendelea Unaendelea

Haujaanza

Haujaanza

2. Ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege (Apron)

i) Ujenzi wa Apron

Haujaanza

3. Ujenzi wa eneo la maegesho ya gari/barabara

i) Ulipaji fidia awamu ya pili

ii) Ujenzi wa eneo la maegesho

iii) Ujenzi wa barabara ya kutoka mjini kwenda jengo jipya

Umemalizika

Haujaanza

Haujaanza

4. Upanuzi wa njia ya kupitia ndege (Taxiway)-Kusini:

i) Hatua ya kusafisha eneo tayari kwa ukaguzi na matayarisho ya malipo kwa wananchi (compensation)

Imekamilika
5.

Uimarishaji wa huduma za Kiwanja cha

ndege cha Abeid Amani Karume:

i) Kuweka viti vipya na imara jengoni

ii) Kuweka vipoza hewa (Air condition)

iii) Kuboresha huduma za vyoo

iv) Kuboresha mazingira/bustani

v) Kuongeza paa sehemu ya kuwasili wageni (Arrival)

vi) Utoaji wa vitambulisho vipya na vyakisasa.

vii) Kuboresha sehemu ya kupokea na kupeleka mizigo uwanjani

viii) Kuweka taa za barabarani

ix) Ufyekaji misitu eneo lote la Uwanja

Imekamilika

Imekamilika

Inaendelea

Inaendelea

Imekamilika

Unaendelea

Imekamilika

Unaendelea

Unaendelea

6. CHANGAMOTO ZINAZOIKABILI MAMLAKA
Ushirikiano na taasisi nyengine ziliopo Uwanjani

2. Madai ya wananchi kwenye maeneo ya Uwanja

3. Utumiaji wa V.I.P

4. Huduma za ZAT

Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali

MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI

Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar, imeanzishwa chini ya sheria No. 3 ya mwaka 2009 (Zanzibar Maritime Authority Act No. 3 of 2009). Mamlaka inamajukumu makuu ya kusimamia sheria Namba 5 ya mwaka 2006 “The Maritime Transport Act. 2006”

1. MAJUKUMU YA MAMLAKA.

Majukumu ya Mamlaka ya Usafiri Baharini ni kusimamia mambo yafuatayo:-

• Kusimamia na kudhibiti shughuli za usajili wa Meli
Ukaguzi na utoaji wa leseni kwa vyombo vidogo vidogo.

• Ukaguzi wa Meli za ndani (TZRS)

• Ukaguzi wa Meli za nje (TZIRS) zinapokuwa katika maeneo ya Zanzibar (Port State Control)
Udhibiti wa safari za baharini kwa Meli na vyombo vidogo vidogo.

• Udhibiti wa uchafuzi wa mazingira ya baharini

• Uchunguzi wa ajali za Meli

• Kusimamia na kudhibiti maslahi na mambo mbali mbali ya mabaharia.

• Utoaji wa leseni za manahodha na wahandisi wa vyombo vidogo vidogo.

• Kutoa hati za mabaharia (discharge book) na vitambulisho vya kimataifa vya mabaharia

• Kusimamia na kudhibiti ulinzi wa Meli ; na Bandari kwa mujibu wa wa sheria za kimataifa “ISPS Code”

• Kusimamia na kuratibu shughuli za utafutaji na uokozi kwa maeneo ya Zanzibar

• .Kusimamia na kudhibiti uondoaji wa mabaki ya meli.

• Kusimamia na kudhibiti taasisi zinazotoa huduma za Meli na Bandari

2. TAARIFA YA UTEKELEZAJI KATIKA KIPINDI CHA MIEZI MITATU DISEMBA 2011 HADI MACHI 2012.

Usajili wa Meli za Ndani

Kwa kipindi cha Disemba 2011 hadi Machi 2012 Mamlaka imesajili jumla ya meli 5 zenye jumla ya uzito wa GRT 5290.04 katika usajili wa ndani kama inavyoonekana kwenye jadweli

DISEMBA 2011

S/NO JINA LA MELI AINA UZITO (GRT)

1. CONDORE CARGO SHIP 943

JUMLA 943

FEBRUARY 2012

S/NO JINA LA MELI AINA UZITO (GRT)

1 RAPTOR(EX PENTOW SALVOR TUG 991

2 SVS MORGAN TUG 863

3 COMARCO 271 HATCH BARGE 1246.52

4 COMARCO 272 HATCH BARGE 1246.52

JUMLA 4347.04

4. USAJILI WA VYOMBO VIDOGO

Mamlaka iliendelea kutoa leseni kwa vyombo vidogo vidogo ambapo jumla ya vyombo 20 vilikaguliwa na kupewa leseni katika kipindi cha Disemba 2011 hadi Machi 2012.

5. NYARAKA ZA MABAHARIA

Katika kipindi cha Disemba 2011 hadi Machi 2012, jumla ya mabaharia 37 walipatiwa vitabu vya ubaharia pamoja na mabaharia 8 kupatiwa vitambulisho vya ubaharia. Aidha jumla ya manahodha 15 walifaulu mtihani na kupatiwa vyeti vya unahodha na jumla ya wahandisi 5 walifaulu mtihani na kupatiwa vyeti.

6. CHANGAMOTO

 Mamlaka inaupungufu wa wataalamu wa kutosha , wenye ujuzi, uzoefu na sifa stahiki katika fani mbali mbali kama vile ukaguzi wa meli, ubaharia, usimamizi na udhibiti wa usalama wa abiria wanaopanda vyombo vya usafiri baharini.

2. Mamlaka inakabiliwa na ukosefu wa baadhi ya kanuni muhimu za Sheria ya Usafiri wa Baharini, namba 5 ya 2006 ili kuwezesha utekelezaji mzuri wa sheria hiyo. Hii inatokana na kutokuwa na fedha za kutengeneza kanuni hizo

3. Ufinyu wa Afisi ya Mamlaka

4. Bajeti ndogo kulingana na matumizi ya Mamlaka

5. Mamlaka inaupungufu wa vitendea kazi kama vili vifaa vya mawasiliano vinavyounganisha Mamlaka na vyombo vya baharini, na taasisi nyengine muhimu za ndani na nje ya nchi.

6. Kutokuwa na uhuru wa kuzitumia fedha zinazoingizwa na Mamlaka kwa ajili matumzi katika kuongeza ufanisi wa shughuli zake.

7. Mamlaka ina jukumu la kusimamia ulinzi na usalama wa Bandari zilizopo Zanzibar. Bandari ya Malindi, Zanzibar inatekeleza matakwa ya kimataifa “Intenational Ships and Port Security code

(ISPS Code) ambayo ni mambo ya kiusalama wa kimataifa. Miongoni mwa changamoto inayoikabili Mamlaka na Bandari hiyo katika utekelezaji wa matakwa hayo ni kutokana na udogo wa Bandari hiyo, kutumia gati kwa meli za kimataifa na meli za ndani na kufanya shughuli za huduma ya mizigo na abiria katika eneo moja kwa wakati mmoja.

8. Kuridhia kwa mikataba ya kimataifa kunakofanywa na Serikali ya Muungano (SMT) hasa katika mikataba muhimu kunarejesha nyuma kutekeleza kwa mambo muhimu, hasa ukuzingatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mamlaka ya Usafiri baharini ndio imesajili meli nyingi za ndani na za kimataifa.

9. Kushindwa kuhudhuria katika warsha, semina, na kozi muhimu za kimataifa kutokana na ufinyu wa bajeti.

Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali.

7. MAFANIKO YA MAMLAKA

1. Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Usafiri Baharini baada ya kuwa kitengo cha kusimamia Usafiri Baharini chini ya Mrajis wa meli

2. Mamlaka imefanikiwa kusajili meli nyingi za ndani (local registry - TZRS) na meli za nje (open registry – TZIRS) katika kanda ya Afika ya Mashariki, ikiwa Zanzibar inaongoza.

3. Kwa mwaka wa fedha 2011/2012 Mamlaka imeweza kuvuka malengo katika ukusanyaji wa mapato zaidi ya asilimia 190.02 ya makisio.

4. Kutoa kwa vitambulisho vya kimataifa vya ubaharia (Seaman ID)

SHIRIKA LA BANDARI

Shirika la Bandari la Zanzibar limeundwa chini ya sheria No.1 ya mwaka 1997.(Act No.1 of 1997).Shirika hili limeundwa kwa kuunganishwa Shirika la Zanzibar Wharf-age na Idara ya Bandari kwa madhumuni ya kuleta ufanisi katika utendaji wa shughuli za kibandari. Majukumu yote yaliyokua yakitekelezwa na taasisi zilizounganishwa sasa yanatekelezwa na Shirika la Bandari.
Shirika hili ni chombo huru cha kisheria chenye maisha ya kudumu na muhuri maalum, uwezo wa kushtaki au kushtakiwa kwa jina lake wenyewe, uwezo wa kununua au kupata kwa njia yoyote ile na uwezo wa kuchukua na kuuza mali yoyote inayohamishika au isiyohamishika kwa ajili ya maslahi ya Shirika.

Kazi na Uwezo wa Shirika

Shirika lina jukumu la kuanzisha kutoa na kurahishisha ushirikiano kuhusiana na mambo ya Gati ambayo yatajumuisha:-

- Maendeleo ya udhibiti wa kutosha wa shughuli za Shirika.

- Kwamba shughuli za Shirika zinatekelezwa kwa ufanisi, kibiashara na huku usalama ukitiliwa maanani.

- Kwamba uthibiti wa fedha za Shirika unafuata masharti ya sehemu ya nne ya sheria ya kuanzishwa Shirika.

- Kwamba Shirika linatoa mambo yote muhimu yanayohusiana na upakiaji, upakuaji na uhifadhi wa shehena na mizigo mengine.

- Kwamba hakuna mtu yoyote au chombo chochote kinachopewa upendeleo au kufanyiwa uonevu usiofaa.

MALENGO YA SHIRIKA

Ndugu waandishi wa habari,

Shirika huwa linajipangia malengo yake kwa mwaka mzima ambapo huzingatia utekelezaji wa kazi za kawaida na kazi za maendeleo kama yanavyopangwa katika bajeti ya mwaka ya Shirika. Utekelezaji wa malengo ya Shirika hutathminiwa katika robo mwaka, nusu, robo tatu na hata mwaka mzima.

Katika kipindi cha Jan – Feb, Shirika limeweza kutekeleza majukumu yake kama ilivopangiwa. Shirika limepokea jumla ya meli 28 za kigeni zenye ujazo wa GRT 359,647.00 vile vile Shirika limepokea vyombo vya hapa nchini jumla ya safari 806 pamoja na majahazi 324. Kwa upande wa makontena Shirika limehudumia makontena 8,856 sawa na teus 11,329 yenye uzito wa tani 119,174.63
Kwa ujumla Shirika limehudumia tani 126,025.05 za mizigo yote iliyowasili na kusafirishwa katika kipindi hicho.

CHANGAMOTO ZA SHIRIKA

Shirika limekabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo uhaba wa vifaa vya kufanyia kazi, Udogo wa Bandari zetu, Mtaji wa kujenga Bandari kubwa ya kibiashara pamoja na wingi wa wafanyakazi katika Shirika lenyewe .

Idara ya Huduma za Bandari - Idara hii imekabiliwa na matatizo ya vyombo vya kuvutia Meli kwani zilizopo hivi sasa kidogo, vichakavu na uwezo wake ni mdogo kulingana na ukubwa wa meli tunazozihudumia Bandarini. Baadhi ya minara na maboya yana matatizo ya taa zake ambapo fedha nyingi zinahitajika katika kubadilisha mfumo wa kutumia taa za gesi na kuelekea katika mfumo kutumia taa za nguvu za jua (Solar).

Idara ya Uendeshaji - Idara hii inakabiliwa na uhaba na uchakavu wa vitendea kazi. Juhudi za Shirika ziko mbioni kuengeza vifaa vipya vya kuendeshea kazi bandarini.

Tawi la Shirika Pemba Tawi limekabiliwa na uhaba wa vitendea kazi katika Bandari ya Mkoani, Maghala ya kuhifadhia mizigo, eneo la kuekea makontena pamoja na kuizungushia uzio Bandari hiyo. Bandari za Wesha na Wete nazo zinahitaji kuengezwa urefu wa kuta zake za gati pamoja na vifaa vya kutendea kazi.

Mafanikio ya Shirika

Shirika la Bandari ni Shirika ambalo halipati ruzuku yoyote kutoka Serikali, hivyo ni Shirika linalojitegemea. Shirika linalofanya biashara kwa faida. Pamoja na kuendesha shughuli za kawaida za Shirika pia hutekeleza kazi za miradi ya maendeleo. Kwa kawaida Shirika huekeza wastani wa Bilioni mbili (2) kila mwaka katika kuimarisha na kujenga upya miuondo mbinu yake.

Shirika limefanikiwa kujenga Chelezo chake, ukuta wa Gati ya Wete, ukutaka wa gati ya Wesha, Afisi ya Bandari ya Wesha, majengo ya abiria ya Bandarini, Wete na Mkoani, Ramp katika Bandari ya Mkokotoni, kukarabati minara yote ya Unguja na Pemba na ufungaji wa taa za nguvu za jua, ununuzi na uekaji wa maboya ya nguvu za jua badala ya gesi, utengenezaji wa Kontena yard ya Bandarini Malindi ujenzi wa ramp ya Landing craft katika eneo la Gati ya Abiria, ununuzi wa Tagi, Boti ya Rubani, ununuzi wa Reach Stacker 2 na Terminal Tractor mbili na hivi sasa Shirika limeshanunua tena Crane nyengine mbili ambazo zinatategemewa kuingia nchini mwisho wa mwezi huu wa machi.

Kwa ujumla Shirika linafanya vizuri katika kunyanyua pato na uchumi wake. Hatua la kuliboresha zinahitajika ili liweze kufanyakazi zake kwa ufanisi na faida zaidi.

Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali.

SHIRIKA LA MELI

1. KAZI ZA KILA SIKU ZA SHIRIKA

Shirika la Meli na Uwakala linafanyakazi zake chini ya uwongozi wa Meneja Mkuu kupitia idara kuu tatu zifuatazo:

- Idara ya Uwakala, Uendeshaji na Masoko

- Idara ya Fedha na Utawala

- Idara ya Ufundi

Mbali na idara hizo, kuna vitengo vingine viwili vidogo ambavyo vipo chini ya Meneja Mkuu ambavyo vinakazi ya kumshauri, vitengo hivyo ni:

- Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Hesabu (internal Audit Unit)

- Kitengo cha Sheria (Legal Office)

A. KAZI ZA IDARA YA UWAKALA, UENDESHAJI NA MASOKO

Idara hii ipo chini ya Meneja Uwakala, Uendeshaji na Masoko na wasaidizi wake wakuu wawili, kazi kubwa za kila siku za idara hii zimegawanywa katika vitengo viwili:

Kitengo cha Uwakala:

Kitengo hiki kinahusika na kufuatilia masuala yote ya huduma za meli za nje zinazowasili katika bandari za Zanzibar.kitengo cha uwakala kinahudumia meli tafauti za kigeni kama vile meli za makontena, meli za mafuta, meli za mchele, meli za kitalii, meli mchanganyiko na meli za magari n.k.

Katika kutoa huduma kwa meli hizo idara hii hufanya makusanyo ya “demurrage” , “ release” , “ commission”, “tally”, na “ watchmen”.

Katika kipindi cha mwezi Disemba hadi Machi 2012, idadi ya meli za nje zilizowasili Zanzibar na kuhudumiwa na shirika zilikuwa 36, ambazo meli za makontena zilikuwa 30, Meli za mafuta zilikuwa 2, meli za mchele 2, meli za utalii 2.

Kiasi cha mzigo kilichoshushwa wa ujumla ni tani 8,000 na mzigo wa mafuta ni 1533.15 Mts.

Kitengo cha Uendeshaji na Masoko:

Kitengo hiki kinahusika na uendeshaji wa meli za ndani za shirika. Kazi yake kubwa ni kuratibu na kuandaa shughuli za upakiaji wa abiria na mizigo, upangaji ratiba wa meli, utafiti na masoko, kutayarisha huduma zote za meli kabla ya na baada ya safari n.k

Amesema hivi sasa, kitengo hiki kinaendesha meli moja tu ya abiria na mizigo (M.V Maendeleo), baada ya kuuzwa kwa meli nyingine nne. Kazi za uendeshaji wa meli nyingine ya mafuta ya shirika (M.T UKombozi) haipo chini ya kitengo hiki kwa vile meli hii imekodishwa kwa kampuni ya Gapco Zanzibar Ltd, kwa mkataba wa “Time Charter” wa mwaka mmoja.

Katika kipindi cha mwezi Disemba hadi Machi 2012, kitengo hiki kimekuwa kikishirikiana na idara ya Ufundi ya shirika, kuifanyia matengenezo meli ya M. V Maendeleo ambayo ilipata maharibiko katika majenereta yake mawili na injini ya “port”. Mnamo tarehe 13/12/2011 meli hii ilipelekwa Mombasa Kenya kwa matengenezo makubwa, baada ya matengenezo hayo meli hii ilianza tena safari zake za kibiashara kuanzia tarehe 18/1/2012.

. IDARA YA UFUNDI

Idara hii inajukumu la kuhakikisha meli za shirika zinakuwa katika hali nzuri kiufundi na kiusalama wakati wote. Kwa hivi sasa idara hii inahudumia meli mbili zilizobaki za M.T Ukombozi na M.V Maendeleo, meli zote hizi ziliundwa mwaka 1980 na sasa zina umri wa miaka 31.

Kazi za kila siku za idara hii ni kuhakikisha kuwa meli za shirika zinakuwa katika hali ya uzima kabla na baada ya safari. Kazi kubwa na ngumu ya idara hii ni kuweza kuchunguza, kubaini na kufanya matengenezo ya vyombo vya shirika hasa ukizingatia kuwa vyombo ni vikongwe na vichakavu na huhitaji matengenezo ya kila wakati kutokana na maharibiko ya mara kwa mara.

Katika kipindi cha mwezi Disemba 2011, meli ya M.V Maendeleo iliharibika kama ilivyoelezwa hapo juu, na idara hii ilifanyakazi ya kuifanyia matengenezo madogo madogo hapa hapa Zanzibar ambayo yalihusisha injini na majenereta na hatimae kupelekwa Mombasa Kenya kwa matengenezo makubwa (dry dock) yaliyohusisha mashine ya ‘star board’, kuweka vipuri vipya na kusafishwa.

Meli hii ilirudi matengenezoni mwanzoni mwa mwezi Januari 2012, ikiwa katika hali ya uzima na hivi sasa inaendelea na safari zake za kibiashara kama kawaida.

Meli ya M.T Ukombozi, inaendelea na shughuli zake za upakizi wa mafuta, katika kipindi cha miezi sita iliyopita imekuwa ikifanyiwa matengenezo makubwa ya majenereta yake mawili na “main air compressor”. Baada ya matengenezo hayo meli ipo katika hali nzuri kiufundi na inaendelea na safari zake za kibiashara chini ya kodi.

C. IDARA YA FEDHA NA UTAWALA

Idara hii inashughulika na masuala yote ya fedha zinazoingia katika Shirika pamoja na matumizi baada ya kupata idhini na taratibu za matumizi ya fedha za serikali. Pia idara hii inahusika na uajiri wa wafanyakazi, mafunzo na utawala.

2. MALENGO YA SHIRIKA
Ndugu waandishi wa habari,

- Kufanikisha juhudi za upatikanaji wa meli mpya

- Kuandaa mpango mpya wa ajira za mabaharia (sign on/sign off)

- Kuendelea na mkakati wa kulifufua upya shirika kwa kuwa na sheria yake na mpango endelevu wa biashara.

3. CHANGAMOTO

- Uchakavu wa meli

- Maharibiko ya meli ya mara kwa mara

- Kuongezeka gharama za matengenezo na uagiziaji wa vipuri

- Upandaji wa bei za mafuta mara kwa mara

- Idadi kubwa ya wafanyakazi

Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali

4. MAFANIKIO YA SHIRIKA

Katika kipindi hiki kifupi shirika limepata mafanikio kiasi katika utendaji wa kazi zake muhimu kama ifuatavyo:

- Kuziweka meli zake katika hali nzuri licha ya uchakavu na ukongwe wake kwa kuzifanyia matengenezo makubwa na madogo.

- Kuendelea kulipa mishahara ya wafanyakazi wake kwa wakati

- Kuendelea kulipa viinua mgongo kwa wastaafu kwa wakati, ambapo katika kipindi hicho cha miezi sita wafanyakazi wawili walistaafu na kiasi cha Tshs. 13.2 milioni kilitumika kuwalipa.

- Kulipa gharama za mafunzo ya wafanyakazi, ambapo katika kipindi cha Julai hadi Disemba 2011, shirika limesomesha wanafunzi 7, wakiwemo mabaharia 3, wafanyakazi wa afisini 4 kwa mafunzo mbalimbali na viwango tofauti. Gharama zilizotumika kwa mafunzo hayo ni Tshs. 11, 142, 500.00

- Kumaliza awamu ya kwanza ya jengo jipya la ofisi ya shirika Pemba.
OFISI KUU PEMBA – MIUNDOMBINU NA MAWASILIANO

Afisi Kuu Pemba ni miongoni kati ya taasisi za Wizara

ya Miundombinu na Mawasiliano – Zanzbar.

Majukumu ya Afisi Kuu – Pemba.

• Kuratibu shughuli zote za sekta za Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kwa upande wa Pemba.

• Kusimamia na kuunganisha Pemba na Makao Makuu

Zanzibar.

• Kuunganisha Wizara na Mashirika yote ya Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano yaliopo – Pemba.

Kazi za Ofisi kuu – Pemba kwa kila siku ni matengenezo ya barabara, kusimamia miradi maendeleo, kusimamia utoaji wa leseni na ukaguzi wa magari, kusimamia masuala ya utumishi pamoja na secta nyengine za wizara..

2.O MUUNDO WA TAASISI.

Afisi Kuu Pemba imeundwa na Taasisi ( idara) zifuatazo:-

Idara ya Uendeshaji na Utumishi, Idara ya Mipango, Sera na Utafiti, Idara ya Utengenezaji na Utunzaji barabara (UUB), Idara ya Usafiri na Leseni, Mamlaka ya Viwanja vya ndege, Idara ya Mawasiliano, Mamlaka ya Usafiri baharini, Shirika la Bandari na Shirika la Meli.

2.1. IDARA YA UENDESHAJI NA UTUMISHI.
Majukumu ya Idara
Idara ya Uendeshaji na Utumishi ina majukumu

yafuatayo:-

• Kusimamia na kushughulikia masuala yote yanayohusu wafanyakazi wa wizara.

• Kusimamia utekelezaji wa sheria ,sera na kanuni za kazi na taratibu mbalimabali za serikali.

• Kusimamia mafunzo na kuandaa mpango wa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kwa wafanyakazi wa wizara.

• Kuandaa taarifa ya mapato na matumizi ya kila mwezi.

• Kusimamia nidhamu za wafanyakazi.

• Kusimamia shughuliza utawala na utumishi.

• Kukusanya na kusimamia mapato yote ya Wizara hapa Pemba.

Malengo ya 2011-2012.

Ndugu waandishi wa habari,

Afisi kuu Pemba kupitia Idara ya U/Utumishi ina malengo ifuatayo:-.

• Kuendelea kuzifanyia ukarabati nyumba za wageni Gombani na kuanzisha ujenzi wa jengo jipya la wageni katika eneo hilo.

• Kufundisha wafanyakazi na kuwaendeleza katika fani mbalimbali.

• Kusimamia masuala ya kiutumishi na uendeshaji.

• Kuhakikisha kuwa mapato tuliyotakiwa kukusanywa na ofisi kuu – Pemba tunafikia lengo.

• Kuendelea kutoa taalum kwa wafanyakazi kuhusu umuhimu wa kujikinga na maambukizo ya virusi vya ukimwi.

• Kuhakikisha kila mfanyakazi anapatiwa majukumu yake.

• Kuingiza wafanyakazi wote katika database.

• Kuwaelimisha wafanyakazi wake ili waweze kupokea mishahara yao Benki.

Mafanikio.

Afisi Kuu Pemba kupitia Idara ya Uendeshaji na Utumishi imefanikiwa katika mambo yafuatayo:-

• Idara imefanikiwa kufanya ukarabati wa ofisi.

• Idara imefanikiwa kuboresha ofisi zake ikiwemo sehemu ya masjala na sehemu ya hesabu kwa kuweka vyombo vya usafiri.

• Afisi kuu – Pemba imefanikiwa kukusanya Jumla Tsh.26,645,130/= kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia Dec hadi Feb 2012.

• Afis kuu – Pemba imefanikiwa kutoa elimu juu ya kujikinga na maambukizo ya ukimwi kupitia warsha pamoja na vipeperushi.

• Afisi Kuu Pemba kupitia Idara ya Uendeshaji na Utumishi imefanikiwa kuwapatia nafasi za mafunzo wafanyakazi wake 10 katika fani mbali mbali.
changamoto.

• Ukosefu na uhaba wa wataalam kwa baadhi ya fani.

• Upungufu wa vitendea kazi.

Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali.

2.2 IDARA YA MIPANGO , SERA NA UTAFITI.

Majukumu ya Idara

Idara ya Mipango,Sera na utafiti ina majukumu

yafuatayo:-

• Kupanga, Kuratibu, kusimamia na kutathimini utekelezaji wa sera na mipango ya maendeleo ya sekta ya usafiri wa baharini,nchi kavu na Anga.

• Kuratibu na kuunganisha Idara zote na Mashirika yote ya Wizara hii.

• Kusimamia ukusanyaji wa takwimu zote zinazohusiana na sekta ya Miundombinu na Mawasiliano.

• Kufanya tafiti mbalimbali za maendeleo katika sekta ya Miundombinu na Mawasiliano.

• Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa shughuli za Bajeti, MTEF, MKUZA na SP.

• Kuratibu kazi za kawaida na maendeleo za wizara.

Malengo.

Ndugu waandishi wa habari,

Afisi kuu Pemba kupitia Idara ya M/Sera na Utafit ina malengo ifuatayo:.

• Kuimarisha vitendea kazi kwa Idara kama vile compyuta na vyombo vya usafiri kwa lengo la kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

• Kuimarisha ofisi ili iwe ya kisasa.

• Kufanya tafiti mbalimbali zinazohusu sekta ya Miundombinu na Mawasiliano.

• Kuandaa miradi ya maendeleo (project Proposal) yanayohusu sekta ya miundombinu na Mawasilino kwa lengo la kufanikisha Mpango Mkakati wa Wizara.

Mafanikio.

• Idara imefanikiwa kusimamia bajeti, MTEF, MKUZA na SP pamoja na ukusanyaji wa takwimu mbalimbali za wizara ya Miundombinu na Mawasiliano hapa Pemba.

• Idara imefanya kazi mbalimbali za kawaida na zamaendeleo.

Changamoto.

• Upungufu wa vitendea kazi kama vile kompyuta.

• Ukosefu wa chombo cha usafiri katika Idara .

• Uhaba wa wataalamu.


Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali.

2.3 .IDARA YA USAFIRI NA LESENI

Majukumu.

Afisi Kuu – Pemba kupitia Idara ya Usafiri na Leseni, ina majukumu yafuatayo:-

• Kuendelea kusimamia usalama kwa watumiaji wote wa barabara, jukumu hilo linahusika na kazi za ukaguzi vyombo vya moto.

• Upasishaji wa madereva na kutoa mafunzo kwa watumiaji wote wa Barabara.

• Kudhibiti utoaji wa huduma za usafirishaji abiria na mizingo kwa njia ya barabara.

• Kufanya matengenezo magari ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar..

• Kufanya mitihani kwa madereva wanaotaka Leseni za Udereva.

• Kupasisha madereva na kuhakikisha kwamba wale wote wanaotaka udereva wamefanyiwa majaribio na kufaulu vizuri na kutoa hati ya umahiri yaani “Certificate of competence”.

• Kutoa learner za udereva.

• Kukusanya mapato kwa kazi zinazofanywa na Idara.

• Kusajili vyuo vya udereva pamoja na kuvisimamia kwa lengo la kuhakikisha upatikanaji wa madereva bora na wa kisasa.

• Kuhakikisha kwamba vyuo vya udereva vinatoa mafunzo yatakayo saidia kupunguza ajali za barabarani.

Mafanikio.:

Katika kipindi cha December 2011 hadi Feb 2012 idara imepata mafanikio yafuatayo:-

• Ukaguzi wa magari, ambapo jumla ya vyombo 1564 vimekaguliwa kwa kipindi cha miezi mitatu..

• Kuhusu upasishaji wa madereva Jumla ya madereva 681 walijaribiwa, waliofaulu na kupewa vyeti vya umahiri ni 520 na waliofeli ni 161.

• Utoaji wa Learner driving licence kwa wale ambao wamejiunga na vyuo vinavyotoa mafunzo ya udereva, ambapo jumla ya Learner 259 zimetolewa .

• Idara imefainikiwa kuimarisha karakana kwa kuongeza vifaa mbalimbali.

• Kufanya matengenezo magari ya serikali..

• Katika kipindi cha Dec 2011 hadi Feb 2012 Idara imekusanya jumla ya Tshs 16,944,500/=

Malengo ya Idara:

Ndugu waandishi wa habari,

Idara ya Usafiri na Leseni ina malengo yafuatayo :-

• Kuimarisha ukaguzi wa kila mwaka kwa vyombo vya moto .

• Kuimarisha mitihani ya madereva kwa kuongeza vyuo vya mafunzo ya udereva.

• Kuongeza uwezo wa kupokea matengenezo ya magari ya serikali pamoja na kuimarisha sehemu ya kiwanda.

• Kuendelea kusajili vyuo vya udereva.

• Kuendeleza ujenzi wa Afisi ya Idara kwa mwaka wa fedha.

• Kusomesha wafanyakazi kwa lengo la kuongeza ujuzi wa utendaji kazi.

Changamoto:

• Magari ya Serikali ambayo yalitakiwa yaletwe karakana ya mitambo hayaletwi ipasavyo.

• Mitambo yote ni chakvu mno.

• Upugufu wa vitendea kazi kama vile compyuta na vifaa vya mitambo..

Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali

2.4 IDARA YA UUB.

Majukumu - Afisi kuu Pemba kupitia idara hii ina majukumu yafuatayo:-

• Kusimamia na kutunza barabara zote za Pemba.

• Ujenzi wa barabara za Pemba.

• Ukarabati wa barabara za Pemba

Malengo ya Idara.
Ndugu waandishi wa habari,

Afisi kuu Pemba kupitia idara ya hii ina malengo yafuatayo:-

• Matengenezo ya barabara zote ili ziweze kupitika muda wote.

• Ujenzi wa barabara ya Mgagadu- Kiwani yenye urefu wa 7.6km.

• Ujenzi wa barabara ya Mkanyageni – Kangani yenye urefu wa 6.5km.

• Ujenzi wa barabara ya Micheweni – Maziwa ngombe – Kiuyu yenye urefu

wa 7.0km.

Mafanikio
Ofisi Kuu Pemba kupitia Idara ya UUB imefanikiwa katika mambo yafuatayo;-

• Matengenezo ya barabara mbali mbali za Pemba yamefanyika kwa kipindi cha miezi mitatu ikiwemo uwekaji wa tabaka la lami 2km kwa barabara ya Weni – Wete, ukataji majani, usafisaji wa misingi kwa barabara mbalimbali za Pemba . Uzibaji wa viraka kwa barabara ya Ole- Konde, Kilindini – Micheweni na Chake – Mkoani. Aidha kazi za Ujenzi wa madaraja na Culvert ziko katika matayarisho kwa daraja la kicha na Pujini.

• Kwa upande wa miradi, shughuli za ujenzi wa barabara unaendelea kwa barabara zinazofadhiliwa na BADEA/ SAUD FUND ambazo ni Wete – Konde na Wete - Gando.

• Aidha mradi wa NORAD unaotumia nguvu kazi ( labour base) umshakamilika na kilichobakia ni kuweka alama za barabarani.

• Ujenzi wa barabara ya Mgagadu – Kiwani unaendelea na hatua iliyofikiwa ni kuweka tabaka la pili la kifusi (subbase) kwa 2 .5 km. Na kazi ya usafishaji imefikia km 4.

Changamoto.
.
. Uharibifu wa zana zinazotumika mara kwa mara kutokana na uchakavu kama vile kijiko, motor grader na roller.

• Kutokufika fedha kwa wakati.

2.5. MAMLAKA YA USAFIRI BAHARINI

Majukumu.

• Kusimamia hali ya usalama wa vyombo vya baharini na idadi ya abiria wanaosafiri kupitia vyomb hivyo.

Mafanikio.

Ndugu waandishi wa habari,
• Mamlaka imefanikiwa kusimamia kazi zake kama ilivyopangiwa.

Changamoto.

• Ukosefu wa vitendea kazi

• Ukosefu wa vyombo vya usafiri ambavyo vitawasaidia kufanyakazi kwa ufanisi zaidi.

2.6 IDARA YA MAWASILIANO.

Majukumu ya Idara.

• Kuratibu na kusimamia uwekaji wa miundombinu ya mawasiliano.
Mafanikio.

• Idara imefanikiwa kufanya ukaguzi wa minara ya mawasiliano hapa Pemba ikishirikiana maofisa kutoka Unnguja.

Changamoto.

• Ukosefu wa vitendea kazi.

• Uhaba wa wataalamu wa ICT.
Wizara inaendelea kukabiliana na Changamoto hizo kwa kuhakikisha kuwa bujeti ya Wizara inaongeza kwa mujibu wa hali ya Fedha ya Serikali

Ndugu Waandishi wa Habari, kwa kumalizia, napenda kuwashukuru kwa ushiriki wenu katika kikao hichi kwani bila ya ushiriki wenu kikao hiki kisingelifanikiwa.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.











No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.