Habari za Punde

Wanamichezo wa Habari Waandaliwa Tafrija Kuwapongeza

 Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdilla Jihad, akitowa shukrani kwa Wachezaji wa timu ya Habari kwa ahadi yao waliompa ya kuleta ushindi katika mashindano ya timu za Habari yanayoandaliwa na NSSF.
Mhe Waziri wa Habari,Utamaduni, Utalii na Michezo Mhe Said Mbarouk, akitowa nasaha zake kwa wachezaji wa timu hiyo kwa kuleta ushindi kwa timu hiyo na kuwa mfano wa Wizara ya habari imefanya kama jina lake la kuonesha ushindi.  
 Viongozi wa timu ya Habari Zanzibar wakimsikiliza Mhe Abdillah Jihad, akitowa nasaha zake kwa Wachezaji hao baada ya kuibuka na Ushindi wa jumla kwa timu zote za Wanaume na Wanawake, akiwa ni mgeni rasmin katika tafrija hiyo na kuwaaga wachezaji na Wafanyakazi wa Wizara hiyo.
 Wachezaji wa timu ya Habari Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Habari, Utamaduni,Utalii na Michezo Mhe Said Mbarouk, akiwapongeza na kujitambulisaha kwao.
 Mdau mambo ya msosi wa kujipongeza kwa ushindi wa jumla kwa timu zao zote za Mpira wa miguu na netiboli, wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Uongozi wa Wizara kwa ajili yao katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani.   

Wachezaji wa timu ya Habari wakijipongeza kwa mlo wa mchana ulioandaliwa kwa ajili yao kusherehekea ushindi wao wa mashindano ya NSSF yaliofanyika wiki iliyopita Mjini Dar-es-Salaam. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.