Na Mwantanga Ame
SERIKALI ya Zanzibar inakusudia kuandaa sheria itayoweka utaratibu utakaoweka uwiano wa mgawano wa nafasi za kazi katika Taasisi zilizo chini ya mambo ya Muungano.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammd, aliyasema hayo barazani jana wakati akijibu swali Mwakilishi wa Kiwani, Hija Hassan Hija.
Mwakilishi huyo alitaka kujua sababu za kutokuwepo uwiano wa uteuzi wa nafasi za Ubalozi nchi za nje.
Waziri Aboud, alisema serikali inajiandaa kuanzisha sheria hiyo ili kuweka uwiano sawa katika nafasi za ubalozi nchi za nje.
Alisema serikali itachukua hatua hiyo kutokana na kuwepo malalamiko katika taasisi mbali mbali zilizochini ya Muungano kwa kukosekana uwiano pale unapofanyika uteuzi wa kujaza nafasi mbali mbali..
Alisema kazi kubwa inayohitajika ni Serikali inaongeza kuwasomesha wananchi zaidi ili nafasi hizo zitapotokea iwe kuna watu ambao wataweza kufaidika na ajira hizo.
Alisema katika kuanda mpango huo, hivi sasa imeanza kuimarisha Afisi ya Mambo ya nje ambapo ina nia ya kujenga jengo jipya.
Akijibu suala la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Kojani, Hassan Hamad Omar, aliyetaka kujua idadi ya wafanyakazi waliopewa ajira katika Wizara ya Mamo ya nchi za Nje wanaotoka Zanzibar.
Waziri alisema Wizara ya Mambo ya Nje hivi sasa ina wafanyakazi 432 ambapo kati ya hao Wazanzibari ni 40 na upande wa mabalozi ni 32 ambapo kati yao wanne kutoka Zanzibar na maofisa ni 35 kati ya hao 10 ni Wazanzibari.
Alisema hivi sasa serikali tayari imesha wapeleka Wazanzibari 10 wenye shahada ya kwanza kujifunza masomo ya diplomasia ili watapohitimu waweze kuajiriwa katika taasisi hiyo.
Aboud, alisema katika kulifanyia kazi hilo, serikali imeteuwa Balozi na Naibu Mwakilishi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
4 Comments
upumbavu! less than 10% Wazanzibari....vunja vunja!!
ReplyDeleteTatizo hata tukipewa hizo nafasi tutapeleka watu ambao sio 'competent' wakati watu makini wamejaa tele!
ReplyDeleteMimi ktk. hilo wala sina huruma! wahadimu nawafahamu, wantaka hizo nafasi ili wachaguane wao kwa wao.
ReplyDeleteHapo ukiuliza ktk hao wanne, wengine wana miaka zaidi ya 15 kila mmoja.
Na usishangae SMZ wakiulizwa wanasema waendelee!
Wakati mwingine kutetea vitu ambavyo wewe ua jamii yako hawafaidiki navyo mm naona ni uzalendo kichaa!
Wahadimu wanaamini watu wa shamba flani flani tuu ndio wanafaa kua mabalozi, huyo mwakilishi angeulizia hao wafanyakazi, Maofisa na Mabalozi na maeneo yao wanayotoka angeshangaa na roho yake,..angesema bora tusipewe!
Jaman haya mwayajua leo jua lishakuchwa, ama kweli ukiwa mwendaadhim hata ukitibiwa utabakia na mapepe tu.
ReplyDelete