Na Hafsa Golo
WANANCHI wa jimbo la Mpendae wametakiwa kuwa na uvumilivu katika kupatiwa huduma za ya jamii kwani ni mambo yanayohitaji mbinu na maarifa katika utendaji na sio kukurupuka.
Wito huo umetolewa na mwakilishi wa jimbo la Mpendae Mohamed Said Dimwa wakati alipokuwa akijibu hoja za wananchi wa Jimbo hilo katika afisi ya gazeti hili.
Alisema kuwa pamoja na ahadi nyingi zilizokuwa wakizitowa katika kampeni lakini cha msingi zaidi wamekusudia kuimarisha mambo ambayo yataweza kulenga jamii na sio mahitaji ya mtu mmoja mmoja kama ilivyozoeleka na watu wengi wa zanzibar hivyo wasibebeshwa lawama kusiana na mahitaji binafsi ya mtu.
Mwakilishi alisema kuwa miundi mbinu ya maji katika jimbo hilo yamekuwa ni chakavu hivyo ni lazima zitumike mbinu mbadala za kuweza kupatikana huduma hiyo bila ya matatizo hivyo wamo katika harakati za kufatilia ili waweze kulitatua suala hilo.
Aidha alisema kuwa watapomaliza kulikwamua suala la maji wanakusudia kujenga skuli ya sekondari katika maeneo ya mpendae na mambo yote yanahitaji ufatiliaji wa kila siku na sio kukaa kitako,hivyo kutoonekana jimboni mara kwa mara ni suala la majukumu ya wananchi waliomkabidhi katika jimbo hilo na sio vyenginevyo kama inavyodhaniwa na baadhi wananchi wa jimbo hilo.
Dimwa aliwaomba wananchi wa jimbo hilo kuwa na moyo wa subira na waache jazba na kuondosha tafauti kili waweze kupata mashirikiano ya pamoja katika kuimarisha mambo ya msingi ambayo yatawaletea maendeleo ya haraka katika jamii na kutatoa matatizo ya ajira kwa vijana wa Jimbo hilo.
Awali wananchi hao walisema wamechoshwa na ahadi hewa za viongozi wao wa Jimbo hilo kutokana na kutotekeleza ahadi hata moja walizokuwa wakiahidi katika kampeni ambazo zilijenga imani ya matumaini katika kuwatatulia kero zao ikiwemo sekta ya ajira kwa vijana ajira, maji salama,elimu na kuweka mazingira mazuri ili kuondokana na maradhi yasio ya lazima jimboni mwao.
Mbali na hayo walisema katika barua yao kuwa hakuna mashirikiano yoyote na viongozi wao wa Jimbo hususan Mbunge na Mwakilishi hivyo wana hofu kukosa fursa ya kutumia haki yoa ya msingi katika kujenga taifa lililo bora na kupata maendeleo ya haraka kama wanavyoona majimbo ya jirani.
Ilieleza barua kuwa kuna matatizo mengi na ni kero kwa wanampendae na wazanzibari kwa ujumla lakini hawaelewi vipi yatafikishwa bungeni kwani muhusika wa kuwasemea hajulikani wapi hasa anapoishi ili wananchi wafikishe malalamiko yao ya kutetea haki zao hivyo imekuwa ni vigumu kapata ufumbuzi kwao.
"Wanampendae tumechoshwa sana na maneno ya uongo,mbunge apite apite jimboni kwake yeye na biashara zake na viwanda vyake vya saruji hayupo kabisa Zanzibar hatujawahi kumuona Mbunge hata mazikoni kero zetu tupeleke wapi huko bungeni kwenyewe hana analosema hakai na sisi tukamueleza matatizo yetu", ilieleza barua.
No comments:
Post a Comment