Hii ni timu machachari ya Kundemba ya miongo mitatu iliyopita ilikuwa ikicheza Central na hatimae daraja la pili. Picha hii ilipigwa mwaka 1984
Kutoka Kulia waliosimama ni Ahmed Nyenye ( Dila nene), Zahran Muazini, Ali Rajab, Ali Juma ( Yupo UK) Ramadhan Hassan ( Manishai), Ali Tall, Juma Sumbu ( Sasa ni Kocha). Waliokaa kutoka Kulia Muhsin, Juma Mkambi, Shaaban Mnyepe, Edi Abushiri, Juma Kikoti ( Marehemu) na Ali Jae ( Yupo UK)
Una kumbukumbu yoyote ya chama hili ambalo lilikuja kufutwa mwaka 1998 baada ya game kati yake na Mwera Star baada ya kutokea fujo uwanja wa fuoni iliyopelekea askari kuingilia kati kwa refa kuipendelea timu ya Mwera dhahir shahir.
Imerudishwa tena miaka miwili iliyopita na majuzi tu ilishuka daraja kutoka daraja pili na kuwa la tatu.
MWENGE WA UHURU WAZINDUA KITUO CHA POLISI NYAKITONTO KWA AJILI YA KUONGEZA
USALAMA
-
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Ismail Alli Issu, amesema
uwepo wa miradi mingi yenye thamani kubwa katika Halmashauri ya Wilaya ya
Kasulu ni...
3 hours ago
No comments:
Post a Comment