Na Emmanuel Siame, AJTC
NYUMBA tatu zimeteketea kwa moto juzi usiku katika eneo la Darajani Mkoa wa Mjini Magharibi na kusababisha hasara kubwa kwa wamiliki wa nyumba hizo.
Mali kadhaa ziliteketea katika nyumba hizo ambapo hadi sasa haijafahamika hasara ya mali zilizokuwa ndani ya nyumba hizo.
Moto huo ambao ulianza kuwaka majira ya saa 12 jioni, uliteketeza kabisa nyumba ya Asha Ibrahim Suma (32), nyumba ya ya Abdul-hamid Mohammed (45) na Radhia Abdalla Juma (64) ambao ni wakaazi wa nyumba hizo.
Akizungumza na Zanzibar Leo kuhusu tukio hilo, Mkuu wa kikosi cha zimamoto na Uokozi, Suleiman Ahmeid Suleiman, alisema kuwa chanzo cha moto huo kilitokana na hitilafu ya umeme katika nyumba moja wapo ya nyumba hizo tatu.
Aidha Suleiman, alisema kuwa moto huo waliweza kuudhibiti baada ya jitihada kubwa ya kulifikia jumba lililoungua, kutokana na gari lao kutopita katika barabara ya njia za mji mkongwe.
mara moja ambapo magari ya zima moto yaliweza kufika mara moja katika tukio hilo nakuweza kulikabili janga hilo lakini hapakuweza kuokolewa kitu chochote kile kutokana na miundombinu ilivyo
Mmoja wa wakaazi wa nyumba hiyo, Asha Ibrahim Suma (32) aliiambia Zanzibar Leo, kuwa alikuwa amekwenda kuswali sala ya Magharibi akiwa amemwacha mtoto aliyewasha televisheni na baada ya muda mfupi alisikia mlipuko katika soketi ya umeme ndipo moto ukaanza kusambaa kwa haraka katika maeneo mengine ya nyumba hizo
Alisema moto huo ulisambaa kwa kasi kubwa na hivyo kushindwa kuokoa chochote baada ya wao.
“Kwa kweli tuliweza kujiokoa sisi kutokana na moto huo kuwaka kwa kasi sana”, alisema
Aidha baadhi ya wamiliki wa nyumba hizo walikuwa hawapo wakati tukio hilo lilipotokea.
“Vitu vyangu vyote viliungua kwa sababu tunalala maeneo mengine na tulipofika baada ya kupata taarifa hatukuweza kufika eneo la tukio”, alisema mmoja wa wakaazi wa nyumba hizo.
Aidha baadhi ya wafanyabiashara katika eneo hilo, wanakusudia kuwachangia wakaazi wa nyumba hizo kwa lengo la kuwafariji.
“Tumekusudia kuweka mchango kwa kila mfanyabiashara wa maduka haya ili tuweze kuwafariji wenzetu,” alisema mmoja wa wafanyabiashara hao ambao hawakutaka kutajwa jina lake.
Gazeti hili lilifanya jitihada ya kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharfibi, Azizi Juma, kutibitisha tukio hilo ambapo bila ya mafanikio ilishindwa kumpata.
No comments:
Post a Comment