Habari za Punde

Uamsho Wasalimu Amri kwa Polisi - Wafuta Mhadhara

Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi Zanzibar 

Wananchi wa Zanzibar wakiwemo wafuasi wa Kikundi cha Uamsho kilichotangaza kufanyika kwa mhadhara kwenye viwanja vya Lumumba mjini hapa, kimetii amri ya Jeshi la Polisi kwa kutoonekana kwa muumini ama viongozi wa kikundi hicho katika viwanja hivyo. 

 Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema leo kuwa, Jeshi la Polisi limeweza kudhibiti maeneo mbalimbali ya mji wa Zanzibar na hivyo kutojitokeza tena kwa wafuasi wa kikundi hicho kama ilivyotangazwa awali. 

Inspekta Mhina amesema Kikundi hicho cha Uamsho kupitia kwa Kiongozi wake Sheikhe Farid Hadi, juzi kilijigamba kufanya Mhadhara mkubwa leo arasili katika viwanja vya Lumumba mjini hapa hata baada ya Serikali kupiga marufuku mikusanyiko, kimeshindwa kufanya hivyo kufuatia agizo la Jeshi la Polisi lakuwataka wasitishe vinginevyo wangekabiliana na mkono wa dola. 


Jana Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Mussa Ali Mussa, alitangaza kuupiga marufuko mhadhara huo na kuwataka wananchi na waumini kutohudhuria na kwa yeyote atakayekaidi agizo hilo angechukuliwa hatua kali.  

Kufuatia agizo hilo, Polisi wa Operesheni maalum leo, walimwagwa katika viwanja vya Lumumba huku magari yenye askari wa kutuliza ghasia yakiranda kwa kila eneo kumkabili yeyote atakayekaidi na kufika kwenye viwanja hivyo kwa madhumuni ya kuhudhuria mhadhara huo. 

Hatua hiyo ya Polisi imeweza kudhoofisha kabisa hali ya majigambo ya viongozi na wafuasi wa Kikundi hicho cha Uamsho waliotangaza kufanya mhadhara huo hata baada ya serikali kupiga marufuku. 

Viongozi wa kikundi hicho ambao walionekana kugawanyika waliwajulisha baadhi ya wafuasi wao kuwa hali isingekuwa swari kwa upande wao kutokana na Jeshi la Polisi kusambaza makachero na askari wa kawaida katika maeneo mbalimbali ikiwemo Viwanja vya Lumumba palipopangwa kufanyika kwa mhadhara huo.

 Ni wafuasi wachache tu walionekana kufika katika msikiti wa Mbuyuni kwa sala ya kawaida na pengine kupata taarifa za hatima ya mhadhara huo uliopigwa stop na Jeshi la Polisi. Mwisho 

 Kwa maulizo wasiliana nami kwa Simu zifuatazo:- 0784 886488, 0715 886488 Insp. Mhina

8 comments:

 1. Kwaiyo,saivi mnatunishiana misuli sio?
  Hakuna yeyote mwenye shida yoyote ya kukuuliza wewe na taasisi yako ya 'wazee wa vyeti feki'!

  ReplyDelete
 2. Nyie Polisi mbwa nyie, na kama msingewapigia magoti Uamsho kusitisha muhadhara tulikuwa tayari na nyinyi kwa lolote, tuliona mlikuwa na silaha za moto, lakini tulikuwa tayari tufe kama si kutunyenyekea, na yule afande wenu "meno ya panya", asingelialia kwa masheikh wetu, tungemuonyesha kuwa hatutishwi na silaha wala kifaru, na wewe Mhina, siku zako za kukaa hapa zinahesabika..jitayarishe kuwa "mwarabu",

  ReplyDelete
 3. haukufanikiwa kufanyika lumumba lakini umefanyka uwanja wa malindi-msikiti wa mbuyuni...na watu wamejaa,,,polisi walizingira.....
  ila ulimaliza salama na watu wakaondoka salamaaaaa

  ReplyDelete
 4. Mwandishi wa Jeshi la Polisi, si ungelingojea kwanza kuliko kukurupuka na pumba zako wakati Mhadhara umefanyika tena hata huyo bosi wako Kamishna Musa ameumwagia sifa. Hii inaonesha wazi kwamba hawa jamaa wa Muamsho ni watu wa Amani na wamekuzidini kete.

  ReplyDelete
 5. wewe ngedere lazima urudi kwenu tanganyika halafu jina la kiislam nani kakubatiza historiya lazima ikuhukumu kama hafiz ali

  ReplyDelete
 6. Mhadhara ulifanyika Mbuyuni. Soma habari hii http://zanzibaryetu.wordpress.com/2012/06/03/mhadhara-wafanyika-kwa-amani/#more-10137

  ReplyDelete
 7. Mtafanya mihadhara sana nyinyi lkn hamfanikiwi!
  Hatupo tayari kutawaliwa na vipofu (watu msioona mbele)

  Wakati vyuo vikuu vinaanza hapa Z'bar , wengi wetu tulikua na matumaini ya kwamba vijana wetu wataelimika, kustaarabika na kuwa na mitazamo ya kisasa lkn. kama comments ninazo ziona kwenye mitandao mbali mbali hapa nchi ndio mawazo ya wahitimu wa SUZA, TUNGUU, CHUKWANI na CHWAKA, tumeumia!

  Katika 'Globalising and civilised world' mtu anafikiria kuwafukuza watu, wakati sisi wenyewe tumetapakaa kila sehemu, na mambo yanakwenda, kwa kweli huyo mtu hatumuhitaji sio tu kama kiongozi lkn hata kama raia. tutamtangaza 'resona non grata'

  Watu wanataka kutuletea mawazo ya 'kiarabu' ili watuharie nchi kama walivyoharibikiwa wao. Nchi za kiarabu zote hazifahamiani wameshindwa kuungana, pamoja na utajiri wote walionao wamegeuka 'nyumbu' akipigwa mmoja wengine wanakimbia!.

  UWAMSHO wanatumia udhaifu na uwezo mdogo wa akili wa watu kuwaambia eti Z'bar itakua tajiri tu kwa kuwa nchi huru bila kueleza mipango au 'potentials zozote za kiuchumi'

  ReplyDelete
 8. WEWE OTHUMAN MAPARA WEWE NA VIKUNDI VYAKONDO MLO CHOMA KANISA MIEMBENI ,TUNAKUJUWENI,NA TUNAO USHAHIDI TOSHA ,MSHAMBA SANA KUMBE WEWE JAMAA, TUNAKUJUWA MPAKA KITANDA UNACHO LALA NA MAKAAZI YAKO YA KARIAKOO ,FALAAAAAAA ASILI YAKO TANGANYIKA UTARUDU KWENU

  ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.