Habari za Punde

Cabo Snoop kupamba ZIFF


Na Asya Hassan
MSANII maarufu kutoka Angola Cabo Snoop, ni miongoni mwa wanaotarajiwa kupamba tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi, linalotarajiwa kuanza Julai 7, mwaka huu ikiwa ni mara yake ya kwanza.

Mratibu wa jukwaa la muziki wa tamasha hilo Hassan Mussa, amesema msanii huyo atashirikiana na wasanii mbalimbali kutoka Tanzania Bara, Zanzibar, Kenya, Comoro, Senegal na Iran.

Aliwataja baadhi ya wasanii watakaoshiriki tamasha hilo kutoka Tanzania Bara, ni Diamond, Banaba, Lina, Sheta, Roma, Kaya, Karora, Kinasha na wale wa Zanzibar ni Sultan King, Sainag, Swahili Vibres, Black Roots, Sekembuke ngoma, na bendi ya Chuo cha Muziki wa Nchi za Jahazi (DCMA).

Aidha muigizaji na muongozaji maarufu wa filamu katika tamasha la Hollywood Mario Van Peeble, atakuwa mgeni wa heshima, kwenye tamasha la mwaka huu ambalo Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.

Mussa ameendelea kulia na changamoto ya kukosa udhamini, na hivyo kutaomba wadau na taasisi mbalimbali za Zanzibar na nje, ili kulipa msukumo tamasha hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.