NAIBU wa waziri
wa Biashara, Viwanda na Masoko, Thuwaiba Edington Kisasi amesema gunia 20 za
karafuu zenye uzito wa kilo 848 zilikamatwa zikitaka kusafisrishwa magendo nje
ya Zanzibar katika msimu uliokwisha.
Naibu waziri
alieleza hayo jana katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi alipokuwa akijibu
suali la nyongeza la Mwakilishi wa Mtambile, Mohamed Haji Khalid aliyeuliza
kiasi cha karafuu zilizokamatwa msimu uliopita zilizotaka kusafirishwa kwa
magendo.
Alisema karafuu
hizo kwanza zilikamatwa zikiwa kwenye vipolo ambapo vilikuwa 31 na zilisafishwa
na baadae kupatikana gunia hizo ambapo kwa baada kupimwa zilikuwa na thamani ya
zaidi ya shilingi milioni 12.7.
Naibu huyo
alisema katika msimu uliokwisha karafu nyingi za magendo zilikamatwa katika
mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akizungumzia
mgao wa fedha zitokanazo na ukamataji wa karafuu za magendo, Naibu huyo alisema
mkoa uliohusika ukamatwaji wa karafuu hizo hupatiwa asilimia 50 ya maunzo.
Aidha alisema
asilimia 20 ya mgao wa fedha zilizokamatwa kwa njia ya magendo hupelekwa kwa
aliyetoa taarifa za magendo, huku asilimia 30 ikipelekwa kwa walioshiriki
kukamatwa kwa karafuu hizo.
Alisema fedha
hizo hutolewa kama kutoa motisha kwa waliokamata karafuu hizo.
No comments:
Post a Comment