Na Haji Nassor, Pemba
WAZAZI na walezi wenye wanafunzi wanaosoma Skuli ya Wambaa Wialya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba,wameiomba Wizara ya Maindombinu na Mawasiliano, kuwajenga matuta maalum karibu na skuli hiyo, ili kuepusha uwezekano wa kutokezea ajali katika eneo hilo.
Walisema, kutokana na barabara hiyo kukamilika kwa kiwango cha lami, imekua ikiwaweka wananfunzi roho juu kwa vile waendesha vyombo vya maoto wamekuwa wakiendesha mwendo wa kasi, hata karibu na skuli hiyo bila ya kujali uwezekano wa kutokezea ajali .
Wakizungunza na mwandishi wa habari hii kwa nyakati tifauti hivi karibuni kijiji huko, walezi na wazazi hao wamesema kuwa, iwapo eneo la karibu na skuli hiyo patajengwa matutu yanaweza kusababisha kwa madereva kupunguza mwendo na kuwapa faraja vijana wao.
Walieleza kuwa kwa sasa hali inatisha, ingawa haijawahi kutokezea ajali ya kugongwa mwanafunzi yeyote, lakini hali iliopo sasa kwa madereva hasa wenye vyombo vya mgurrudumu mawili inatishia usalama wa wanafunzi wao.
Wazazi na walezi hao walizidi kueleza kuwa ni vyema kwa Wizara husika, ikalifanya hilo kwa haraka kabla hapajatokezea madhara yoyote, kwani matatu kwa kiasi kikubwa yanawafanya madereva kupunguza mwendo.
Mmoja kati ya wazazi hao Mohamed Juma, alisema kinachowafanya madereva kwenda mwendo wa kasi ni kutokana na kutokuwa na kizuizi chochote kwenye barabara hiyo jambo ambalo linaweza kusababaisha ajali zisizokuwa za lazima.
‘’Maderava wetu wako huru kwenda mwendo waupendao, maana hakuna kituo cha Polisi na wala kizuizi chochote hata hapa karibu na skuli ambapo wanafunzi hucheza michezo ya kufukuzana’’,alieleza mzazi huyo.
Nae Asha Mohamed alisema anashangaa kuona barabara hiyo na nyengine zimefunguliwa zikia hazijakamilika kwa kutokuwepo kwa alama za barabarani (road sign) ambazo kwa baadhi wakati huwapa alama muhimu maderava.
‘’Alama za barabarani ni miongoni mwa jambo muhimu katika kupunguza ajali za barabarani lakini hii barabara yetu ya Mizingani- Wambaa mwanzo hadi mwisho hakuna alama za barabarani na tayari imeshafunguliwa’’,alizidi kufafanua.
Aidha wazazi na walezi hao walisema iwapo Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano haitoharakisha uwekaji wa matuta na alama za barabarani kwenye barabara hiyo kunaweza kukajitokeza ajali zisizokuwa za lazima.
Hivi karibu Afisa Mdhamini Wizara hiyo Pemba Hamad Ahmed Baucha wakati akizungumza na mwandishi wa habari hii ,alisema kuwa suala la uwekaji wa alama za barabarani Wizara imeshafikia pahala pazuri na wakati wowote hili litafanyika.
Alisema ni kweli barabara hiyo na nyengine tano zimefaunguliwa zikiwa hazina alama za barabarani, na kuahidi hilo kufanyika na kuwataka madereva wanapoingia barabara za ndani kupunguza mwendo ili kuepusha ajali.
Wakati huo huo Kamanda wa Polisi Jamii shehia ya Chumbageni Wambaa Shaaban Jabir alisema wanatarajia kuweka vituo maaluma (block) kwenye barabara hiyo ili kuwataka madereva kuounguza mwendo.
Alisema hata wao kama Polisi jamii suala la baadhi ya madereva kuendesha vyombo vyao kwa mwendo wa kasi hasa maeneo yenye mkusanyiko wa watu kama vile sokoni na skuli limekua likiwaumisha kichwa.
No comments:
Post a Comment