Habari za Punde

Mafunzo: Hatukutumia mamluki ‘Kagame Cup’


Na Shomari Hamad
 
TIMU ya soka ya Mafunzo, imekanusha madai kuwa kiwango kikubwa ilichoonesha kwenye michuano ya Kagame mwaka huu, kilitokana na kutumia wachezaji mamluki.
 
Katibu wa timu hiyo Makame Fadau, amesema wanandinga wote walioichezea katika ngarambe hizo zilizofanyika Dar es Salaam miezi miwili iliyopita, ni wa timu hiyo isipokuwa mmoja tu, Suleiman Kassim ‘Selembe’.
 
Selembe aliyetokea Mafunzo kwenda Azam FC, sasa amesajiliwa na wakata miwa wa Turiani Morogoro, timu ya Mtibwa Sugar.
 
Katika hatua nyengine, Fadau amesema tayari wamemaliza kazi ya usajili na wameshawasilisha ZFA majina ya wachezaji waliosajiliwa na timu hiyo kwa ajili ya kuichezea katika ligi kuu msimu ujao.
 
Aliwataja nyota hao kuwa ni, walinda mlango Khalid Mahadhi kutoka JKU, Salum Mohammed, Suleiman Janabi na Ali Suleiman, ambapo mabeki ni Said Mussa, Yussuf Makame, Maulid Mussa, Ali Juma, Haji Abdi, Hussein Rashid, Hassan Ahmada, Kheir Salum na Juma Othman ambaye ametokea Jamhuri.
 
Viungo ni Mohammed Abdulrahim, Masoud Hamad, Fikirini Rajab, Wahid Ibrahinm, Saleh Ali, Mbarouk Zahran, Salum Said Shebe, Haji Ramadhan na Nassor Mfaume.
 
Fadau aliwataja washambuliaji kuwa ni Jaku Juma Jaku, Bakari Ayoub, Sadik Habib, Zahor Salim na Ali Othman ambaye amenyakuliwa kutoka Jamhuri.
 
Katibu huo amefahamisha kuwa, wameamua kuweka mambo hadharani ili kukata kiu ya wapenzi wake walikuwa wakisubiri kwa hamu kujua kukijua kikosi chao hicho, na pia kuepuka utata wa mchezaji mmoja kusajiliwa mara mbli. 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.