Na Mwantanga Ame
BARAZA la Wawakilishi limetangaza majina ya Wajumbe tano Baraza la hilo wataounda kamati teule itakayochunguza matatizo ya migogoro ya ardhi katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.
Spika wa Baraza la Wawakilishi, Pandu Ameir Kificho alieleza hayo jana wakati akitoa taarifa kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kabla ya kuaghirishwa kikao cha Baraza hilo kilichodumu kwa kipindi cha mienzi miwili hivi sasa.
Spika Kificho alisema Baraza hilo wakati likiendelea na mjadala wa katika wizara ya Ardhi, Makaazi, Maji na Nishati serikali ilikubali kuundwa kwa kamati teule ili kuchunguza migogoro ya ardhi iliyojitokeza katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba.
Alisema serikali imeridhia hilo baada ya wajumbe wa Baraza kuomba kuundwa kwa kamati hiyo baada ya kuwepo malalamiko mengi juu ya suala la mizozo ya ardhi ndani ya mjadala wa wizara tofauti zilizowasilisha bajeti zake.
Alisema ingawa mjadala huo uliopokuwa ukiendelea juu ya suala hilo Mjumbe aliependekeza kuundwa kamati teule, Mbarouk Wadi Mtando, hakuwa na hoja rasmi juu ya suala hilo, lakini serikali ilikubali kuundwa kwa kamati hiyo.
Alisema kutokana na wazo hilo, Baraza hilo, limeamua kuunda kamati hiyo itayokuwa na wajumbe akiwemo Mwakilishi wa Abdalla Juma Abdalla Mwakilishi wa jimbo la Chonga, Nassor Salim Ali Mwakilishi wa jimbo la Rahaleo, Ali Mzee Ali, Fatma Mbarouk Said na Abdalla Mohamed.
Kificho alisema wanatarajiwa kuzifanyia kazi kwa miongozo ya hadidu rejea 12 bila ya kugusa maeneo yenye migogoro ambayo kesi zake zipo mahakamani.
Akitaja hadidu rejea hizo za kuzifanyia kazi Spika huyo alisema ni kuchunguza na watu waliopewa umiliki wa ardhi bila ya kuzingatia taratibu za kisheria na maeneo yaliokuwa yanatumiwa na wananchi kwa shughuli zao za maisha lakini hivi sasa wamenyanganywa.
Aidha, hadidu rejea nyengine alizozitaja Spika Kificho, alisema ni pamoja na Wawekezaji wanaochimba mchanga katika maeneo ambayo yameonekana kuwa na mgogoro wa ardhi baina ya wananchi na wawekezaji hao.
Vile vile Spika huyo alitaja hadidu rejea nyengine ni zinazohusu mgogoro wa ardhi iliotokana na kati ya wananchi na wafanyabishara na maeneo walionyanganywa wananchi na kufanywa ni ya vitega uchumi.
Pia Spika huyo alisema Wajumbe hao wataifanyia kazi migogoro wa ardhi kati ya wananchi na serikali eneo la Mchangamle, mgogoro wa ardhi wananchi na viongozi wakuu wa serikali eneo la vitongoji, Wanavijiji na wawekezaji eneo la Pwani Mchangani.
Akiendelea kutaja maeneo mengine alisema ni unaohusu mgogoro wa Ardhi kati ya viongozi wajuu wa serikali eneo la Tondooni Kisiwani Pemba, mgogoro wa ardhi Tumbe kati ya serikali na wananchi na Mgogoro wa ardhi eneo la Bwejuu
Spika huyo, aliwataka Wajumbe hao kuona wanafanya kazi kwa uadilifu na kuzingatia sheria ili kuweza kupatikan kwa taarifa ya msingi juu ya migogoro hiyo ili kuweza kuisaidia serikali.
No comments:
Post a Comment