Habari za Punde

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari Zanzibar

SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
WIZARA YA HABARI UTAMADUNI UTALII NA MICHEZO



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Idara ya Habari(MAELEZO) tunawakumbusha tena waandishi wa habari juu ya ulazima wa kuwa na kitambulisho cha kufanyia kazi ya uandishi wa habari Zanzibar kilichotolewa na Idara ya Habari Maelezo(Press Card) kwa mujibu wa sheria Zanzibar.

Aidha, waandishi wa habari kutoka nje ya Zanzibar hawataruhusiwa kufanyakazi ya uandishi wa habari mpaka pale amepata ruhusa ya Idara ya Habari Maelezo kwa mujibu wa sheria ya usajili magazeti N0 5 ya mwaka 1988 ya Zanzibar.

Kutokana na hali ilivyojitokeza hivi sasa duniani, tunashauri vyanzo vya habari ikiwemo viongozi wa Serikali wakiwemo Waheshimiwa Mawaziri, Naibu Waziri, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Mikoa na Wilaya pamoja na wasemaji katika Taasisi mbalimbali kutotoa taarifa zozote kwa vyombo vya habari kwa mwandishi ambaye hana Press Card iliyotolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Hivyo, kuanzia tarehe 1/09/2012 waandishi wa habari wote wakiwa kazini ni muhimu kuonyesha kitambulisho kilichotolewa na Idara ya Habari Maelezo.

Aidha,, tunasisitiza kwamba kwa mujibu wa sheria ya usajili wa magazeti sheria N0 5 ya mwaka 1988,kifungu cha 13 kinasisitiza kwamba mtu yeyote atakayechapisha Kitabu, Magazeti, Vipeperushi, Vijarida,Ramani na Chati lazima awasilishe nakala tatu si zaidi ya siku 14 baada ya kuchapishwa kwa Mrajis Idara ya Habari Maelezo Zanzibar.

Kutofanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria ya Usajili Magazeti na Vitabu N0 5 ya mwaka 1988 hatua za kisheria zitachukuwa kwa atakayekiuka.

IMETOLEWA NA:
IDARA YA HABARI(MAELEZO) ZANZIBAR
09/08/2012



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.