Habari za Punde

Uchunguzi wa ajali ya Mv Skagit waanza


Aidan Mhando na Zakhia Abdallah

Tume ya uchunguzi wa ajali ya Mv Skagit iliyozama July 18 mwaka huu imeanza  kuchunguza chanzo  cha ajali hiyo kwa kuwahoji ndugu na jamaa wa abiria waliokuwamo katika meli hiyo.Kazi ya kuwahoji ndugu hao ilifanyika jana katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam huku waandishi wa habari wakizuiwa kuingia ndani ya chumba cha mahojiano.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya chumba hicho cha mahojiano kilieleza kwamba mahojiano hayo yalikuwa yanahusisha makundi mawili, kundi la kwanza lilihusisha Watu ambao hawakupata maiti za ndugu zao na kundi la pili lilihusisha watu ambao walizipata na kuzizika.Chanzo hicho kilibainisha kwamba mmoja wa watu   aliyekuwepo katika mahojiano hayo ni mdogo wa mmiliki wa meli hiyo ambaye hata hivyo jina lake halikufahamika.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa nyakati tofauti ndugu wa abiria ambao walikuwapo katika meli hiyo na kupoteza maisha Omari Saidi alisema wao kama ndugu walitakiwa kufika katika ofisi hizo kutoa maelezo kama walifanikiwa kuwapata ndugu zao.Alisema baada ya kufika waliambiwa kwamba wanatakiwa kuingia ndani kwa makundi ambapo kila kundi moja lilihusisha watu wanne.

“Hapa tuliambiwa tuje kutoa maelezo kama tulifanikiwa kuwapata ndugu zetu na kuwazika au tuliwakosa lakini walikuwapo katika ajali hiyo,” alisema Saidi na kuongeza

“Mfano mimi nilipoteza ndugu zangu wawili mmoja akiwa mama yangu mzazi na mjomba wangu na nilipo ulizwa niliwataja na majina yao yalionekana katika orodha ya watu waliokuwapo katika meli hiyo,” alisema.

Saidi alifafanua kwamba kila mtu ambaye alikuwa anaingia na kutoa maelezo alipewa Sh3000 kama nauli ya kurudia nyumbani jambo ambalo liliwashangaza.“Tumeshangaa sana baada ya kuhojiwa na kutoa maelezo tulipewa Sh3000 kama nauli jambo ambalo najiuliza kwa nini watupe hiyo fedha,” alisema.
Hata hivyo baadhi ya wahanga wa ajali hiyo walidai hawana uhakika watu waliozika kama ni ndugu zao


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.