Makamo Waziri Mkuu wa China Hui Liangyu anatarajiwa kuwasili Zanzibar Tarehe 6/9/2012 kwa ziara ya siku mbili.
Kwa mujibu wa Ratiba iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Tanzania, imeeleza kuwa mara tu atakapowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume atapokelewa na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
Makamo wa Waziri Mkuu huyo wa China Hui Liangyu kwenye Uwanja huo wa Ndege atajulishwa na mwenyeji wake kwa Viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakiwamo Mawaziri na pia kuvishwa Shada la Mauwa na kuangalia ngoma za utamaduni za Zanzibar.
Baadae ataelekea Ikulu ya Zanzibar ambapo atakutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DKT Ali Mohamed Shein na kuwa na Mazunguzo nae na baadae kutia saini makubalianoyatakauoshuhudiwa na Makmao wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd.
Usiku Makamo Waziri Mkuu wa China atahudhuria katika Chakula cha Usiku kilichoandaliwa kwa ajili yake na Mwenyeji wake Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd huko katika hoteli ya La Gemma.
Tarehe 7/9/2012 mgeni huyo atatembelea katika Mji Mkongwe ambapo ataanzia katika Kanisa la Anglican Mkunazini na baadae Beit -el Ajaib na Jumba la Wanaachi la Forodhani na Kuelekea Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kwa kuondoka.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR
No comments:
Post a Comment