Diwani wa Mzuri Kaja Makunduchi, Bi Zawadi Hamdu Vuai akimvisha Meya wa Kiruna Bi Christina kanga ya kisutu. Hii ni kuonyesha heshima ya Zanzibar
Mfanyabiashara wa Kiruna bwana Mats ambaye ameonyesha hamu kubwa kuja Makunduchi kuwekeza katika hoteli. Katika mazungumzo alisema anapenda kufanya biashara zaidi kuliko kuoa
KUTEMBEA
NI CHUO KIKUUNA MOHAMED MUOMBWA KUTOKA KIRUNA SWEDEN
Ziara ya ujumbe wa
wadi za Makunduchi katika Manispaliti ya Kiruna nchini Sweden
inatoa mafunzo mengi kwa Wazanzibari, kati ya mafunzo hayoni ubunifu ni mali na mambo
mengi yanawezekana tukijipanga vizuri.
Safari ya madiwani wa
Makunduchi wakiongozwa na Afisa tawala ndugu Abdallah Kombo nchini Sweden
imekuja kufuatia makubaliano ya awali yaliyofikiwa ya mashirikiano kati ya manispaliti ya
Kiruna na wadi za Makunduchi.
Pande hizo mbili zimekubaliana kushirikiana katika mambo
ya utalii unaojali mazingira pamoja na elimu.
Lakini mashirikiano haya hayakujatu kama mvua.
Hapa ndipo ule usemi usemao hakuna kisichowezekana unapofaa.
Wadi
za Makunduchi baada ya kutafakari zimegunduwa kuwa katika ulimwengu huu wa utandawazi kazi ya kuunganisha nchi kwa nchi
si lazima kufanywa na balozi.
Kwa lugha nyengine diplomasia katika karne ya utandawazi sio milki tena ya mabalozi na ndio maana wadi za Makunduchi zikaamua kutafuta ushirikiano na sehemu
moja wapo ya nchi ya Sweden.
Matokeo ya jitihada hizi zilizoendeshwa kwa mawasiliano ya mtandao ni
kuzaliwa kwa mashirikiano baina ya Manispaliti ya Kiruna n awadi za Makunduchi.
Ujumbe wa manispaliti ya Kiruna
ukiongozwa na bwana Ove ulifanya ziara ya siku nne Makunduchi wakati wa
kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Ziara hiyo ilikuwa na lengo la
kuona maendeleo yetu kielimu na utalii kwa jumla ili kupata picha kamili ya namna
nzuri ya kushirikiana.
Wakati wana Kiruna wakiwa Makunduchi, pamoja na mambo mengine,
walitembelea sehemu ya ukanda wa utalii Paje, Bwejuu na Jambiani kwa upande wa Kusini.
Kwa upande wa Kaskazini walitembelea Nungwi na Kiwengwa.
Jambo jengine lililopelekea wadi za Makunduchi kutoka nje ya mipaka yake
ni kuitikia wito wa Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein unaoutoa kila
siku kuwa wakati umefika wa watu wa Zanzibar
kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea. Kwa lugha nyengine rais wa Zanzibar
anawataka wananchi kuwa wabunifu katika utendaji wao wa kazi.
No comments:
Post a Comment