Na Hafsa Golo
MJUMBE wa Baraza Kuu la Uongozi CUF na Mwakilishi wa Mjimkongwe, Ismail Jussa Ladhu amesema bado balozi za Tanzania nchi za nje hazijautangaza ipasavyo utalii wa Zanzibar.
Jussa alisema moja ya sababu zinazochangia hali hiyo ni kukosekana kwa maafisa na mabalozi kutoka Zanzibar.
Alisema hayo alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho katika mkutano wa hadhara kuukaribisha mwaka mpya uliofanyika Kwambawala.
Alisema katika ofisi nyingi za kibalozi hakuna Wazanzibari jambo ambalo limekuwa likisababisha mabalozi kuwa na kigugumizi cha kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyopo Zanzibar.
Alisema kama mabalozi hao, wangeutangaza utalii wa Zanzibar , Zanzibar ingekuwa ikipokea idadi kubwa ya watalii kuliko nchi nyengine yoyote duniani kutokana na mandhari yake.
Jussa alisema kwa kawaida nchi za visiwa mara nyingi hutegemea zaidi maendeleo ya uchumi wake kupitia sekta ya utalii na biashara kupitia bandari.
Kuhusu maoni ya katiba mpya ya Tanzania, Jussa alizihimiza taasisi za kijamii kushiriki kimalifu katika zoezi hilo.
Alihimiza umoja, amani na mashirikiano kwa wananchi wote ili Zanzibar iendelee kuwa kisiwa cha amani na kimbilio la watalii.
Naye Kaimu Naibu Katibu Mkuu, Salumu Bimani aliwataka wananchi kutoa taarifa kwa taasisi husika pale wanapoona dalili za kutokea vitendo vya kihalifu.
Kutangaza utalii hakuhitaji sana kuwa mzanzibari bali kuwa na maafisa wenye utaalam wa kazi ya kutangaza utalii na vivutio vyengine. However, the main ground work ya kuutangaza utalii wa zanzibar ipo mikononi mwa kamisheni ya utalii, shirika la utalii na wadau wengine wa sekta hiyo. Kinachopaswa kufanywa ni vyombo hivyo kulenga maeneo wanayotaka kuhimiza kampeni za kutafuta soko na ofisi zetu za balozi zitashiriki kutayarisha au kuwezesha utangazaji huo kufanyika. Unaweza kuwa na maafisa wa ubalozi kutoka zanzibar lakini kama hakuna mipango endelevu kutoka kwenye vyombo vinavyosimamia utalii zanzibar ni kazi bure.
ReplyDeleteKauli kama hizi ambazo hazijafanyiwa utafiti zinapoelezwa kwa wananchi zinaweza kupotosha umma. Ombi langu ni kwa hawa wanaeneza chuki dhidi ya Tanzania wajiulize kama wanauzalendo wa kweli na pia wasitumie uchochezi huo kama njia ya kujipatia mtaji wa kisiasa.