Na Abdi Suleiman, Pemba
WALIMU kisiwani Pemba
wametakiwa kuitumia lugha ya alama katika ufundishaji wao maskulini ili
wanafunzi wenye viziwi waweze kufaidika.
Wito huo umetolewa na Afisa Elimu
Mjumuisho Pemba, Hamad Othman Hamad, wakati akizungumza na walimu kutoka skuli
10 kisiwani hapa, pamoja na wanafunzi wao, katika skuli ya Michakaani.
Alisema walimu ni watu muhimu wa
kuweza kuwasaidia wanafunzi wenye uziwi, wanapokuwa madarasani, iwapo
wataitumia ipasavyo lugha ya alama.
Hata hivyo, aliwataka wazazi kuacha
tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu na badala yake wawapeleke skuli kwani
kupata elimu ni haki yao
ya msingi.
Kwa upande wake mwalimu, Raya Said
kutoka skuli ya Minungwini, alisema mafunzo hayo, yatawasaidia katika
ufundishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
Naye mwalimu, Rahma Issa Ali,
kutoka skuli ya Jadida, alisema mafunzo hayo yalikuwa yakihitajika kwa muda
mrefu maskulini katika ufundishaji wa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
No comments:
Post a Comment