Habari za Punde

Jaji Mkuu Zanzibar Azungumza na Waandishi Kuhusi Wiki ya Sheria. Habari

 Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu,akizungumza na Waandishi mbalimbali walioko Zanzibar kuhusiana na Wiki ya Sheria inayotarajiwa kuadhimishwa 7, Feb 2013. Zanzibar na kauli Mbiu ya Mwaka huu ni Kuondosha Udhalilishaji Watoto Kijinsia Zanzibar, mkutano mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ya Jiji Mkuu Mahakama Kuu Zanzibar. 
 Mhe. Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu akisisitiza jambo wakati akizungumza na Waandishi kuhusiana na shughuli mbalimbali za Mahakama na uendeshaji wa Kesi za Udhalilishaji wa Watotona mwenendo wa kesi hizo na kesi mbalimbali.
 Mrajisi wa Mahakama Zanzibar Goerg Kazi akijibu suwali lililoulizwa na Waandishi kuhusiana na mwenendo wa Mahakama Zanzibar, wakati wa mkutano na waandishi kuhusiana na matayarisho ya wiki ya Sheria Zanzibar inayotarajiwa kuadhimishwa siku ya 7-Feb-2013 Zanzibar.
 Waandishi wa habari wakimsikiliza Jaji Mkuu wa Zanzibar, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi.

Mwandishi wa Redio Zenj Fm Moza Saleh akiulisa Swali.
Mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe Mwinyi Sadala akiuliza Swali katika Mkutano huo

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.