Habari za Punde

Waislamu Wahimizwa Kudumisha Amani


Na Fatuma Kitima,DSM
WAISLAMU nchini wametakiwa kuendelea kuishi kwa ushirikiano baina yao na watu wa dini nyengine ili kuendelea kudumisha amani na kujenga upendo.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam katika kongamano la utamaduni la Afrika.

Akizungumza katika kongamano hilo kwa niaba ya Makamu wa Rais, Waziri wa Maji Dk. Jumanne Maghembe alisema waislamu hawanabudi kuhakikisha wanalinda amani kwa kuwa dini hiyo imesisitiza amani.

Dk.Maghembe alisema kuna baadhi ya waislamu wanaotumia kivuli cha dini kuleta vurugu jambo ambalo alisema sio zuri na ni kwenda kinyume na maagizo ya dini hiyo kwani msingi wa uislamu ni amani.

Alisema vurugu sio nzuri katika nchi kwani zinaweza kusababisha uvunjifu wa amani na wakati mwingine kusababisha mauaji.

Hata hivyo, alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwalea watoto katika maadili mema ili kujenga taifa lenye upendo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.