KAULI YA SERIKALI BUNGENI KUHUSU TAARIFA YA AWALI YA TUME YA TAIFA YA KUCHUNGUZA MATOKEO YA MTIHANI WA TAIFA WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012
UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa Spika,
kwa mujibu wa Kanuni ya 49(1) ya Kanuni zaKudumu za Bunge, Toleo la mwaka 2007, naomba kuwasilisha Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya kuchunguza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012.2.
Mheshimiwa Spika,
Waheshimiwa Wabunge watakumbuka kuwa Matokeo ya Mitihani ya Kidato cha Nne mwaka 2012 yalionesha kuwa kiwango cha ufaulu kimeshuka kwa kiwango kikubwa ikilinganishwa na miakaya hivi karibuni.
Matokeo yaliyotangazwa mwezi Februari, 2012 yalionesha kwamba kati ya Wanafunzi
367,756
waliofanya mtihani huo, Watahiniwa
126,847
ndio waliofaulu. Katika idadi hii, Wanafunzi waliofaulu katika Daraja la
Kwanza
hadi la
Tatu
ni
23,520,
sawa na Asilimia
6.4
na Daraja la
Nne
ni
103,327
, sawa na Asilimia
28.1
.
Watahiniwa
240,909
, sawa na Asilimia
65.5
ya Wanafunzi wote waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012 walipata Daraja la
Sifuri
.
3.
Mheshimiwa Spika,
kushuka kwa kiwango cha ufaulu kulihusu shuleza aina zote, yaani Sekondari za Serikali ikijumuisha zilizojengwa kwa nguvuza Wananchi, Shule Binafsi na Seminari.
Takwimu zinaonyesha kwambaukilinganisha matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2011 na mwaka 2012, Shule za Wananchi matokeo yao yameshuka kwa Asilimia
1.82
; Shule za Umma za zamani (Kongwe) yameshukwa kwa Asilimia
6.43
; Shule Binafsi yameshukakwa Asilimia
6.39
; na kwa Shule za Seminari yameshuka kwa Asilimia
7.29
.
Hali hii inaonyesha kwamba, matokeo katika
Shule za Wananchiyameshuka kwa kiwango kidogo
ikilinganishwa na yale ya
Shule zaUmma za zamani (Kongwe), Shule Binafsi na Shule za Seminari
ambazo zilitegemewa kufanya vizuri zaidi ya zile za Wananchi ambazo
matokeo yao
yameshuka zaidi
kwa kati ya Asilimia
6.4
na
7.3
.4.
Mheshimiwa Spika,
kutokana na matokeo hayo yasiyoridhisha naambayo yapo nje kabisa ya mwenendo wa ufaulu kwa miaka ya karibuni,Serikali iliamua kuunda Tume ya Kuchunguza Kushuka kwa Kiwango chaUfaulu wa Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 kwa madhumuniya kupata ufumbuzi wa kudumu.
a)
MMEM I
ambayo ililenga katika kufungua Shule zaidi iliWanafunzi wengi wa rika lengwa waweze kujiunga na Elimu yaMsingi;
b)
MMEM II
ambayo ililenga katika kuboresha ubora wa elimuitolewayo katika Shule za Elimu ya Msingi; na
c)
MMEM III
ambayo ililenga katika kuendelea kuimarisha ubora waElimu ya Msingi baada ya mafanikio ya
MMEM I
na
MMEM II
.
2.Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) wa mwaka 2004ambapo:
a)
MMES I
ambayo ililenga katika kufungua Shule zaidi za Sekondarikatika ngazi ya Kata ili Wanafunzi wengi zaidi wanaomaliza Elimuya Msingi waweze kujiunga na Elimu ya Sekondari Kidato chaKwanza; na
b)
MMES II
ambayo ililenga katika kuendelea kuimarisha ubora waElimu ya Sekondari kadri Idadi ya Wanafunzi wa Elimu yaSekondari wanavyoendelea kuongezeka.
Changamoto zinazoambatana na mafanikio haya ni pamoja namazingira yasiyoridhisha ya kufundishia na kujifunzia, ikiwemo upungufu wa miundombinu muhimu ya shule kama vile Madarasa,Maabara, Madawati, Maktaba, Nyumba za Walimu, Hosteli na majengo mengine muhimu ya Shule.
Vilevile, kuna tatizo la uhaba wa Walimu,Vitabu, zana za kufundishia na matatizo ya Ukaguzi wa Shule. Vilevile, Tume imebaini kuwa Mfumo wa Elimu ya Msingi na Sekondari unakabiliwa na changamoto nyingine mbalimbali ambazo Taifa inapitia kwa sasa ikiwemo masuala ya Kisera, Kisheria, Kimfumo, Kimuundo pamoja na changamoto za uhaba wa Rasilimali Fedha na RasilimaliWatu.
Tume inaendelea kufanyia kazi maeneo haya kwa kushirikiana naWataalamu na Wadau wengine;
6.2Kuhusu matokeo ya Kidato cha Nne mwaka 2012, Tume imebaini kwamba, pamoja na Wanafunzi hawa kuwa katika mazingirayanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita na kwamba ufanisi katika shule kwa ujumla umekuwa unashuka kwa sababu mbalimbali,ufaulu wao umeshuka zaidi kwa sababu ya mabadiliko ya mchakato wakuandaa na kutoa matokeo ya mtihani kwa mwaka 2012.
Mfumouliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.
Uchunguzi unaonesha kuwa mwaka 2011, Baraza la Taifa la Mitihani lilikuwa
linachakata Alama za mwisho kwa kutumia mfumo ambao ulikuwa unabadilika kutegemea hali ya ufaulu wa Mwanafunzi
ambao ni
“National Mean Difference
” (
NMD
).
Utaratibu huu ulitokana natofauti ya Wastani wa Kitaifa wa Alama za Maendeleo kutoka Alama za Maendeleo Endelevu (
Continued Assessment – CA
) za Watahiniwa wote na Wastani wa Kitaifa wa ufaulu wa Mitihani ya mwisho kwa somo husika.
Kila Mtahiniwa aliongezewa
“National Mean Difference
”iliyokokotolewa katika Alama za Mtihani wa mwisho ili kupata Alama
4
itakayotumika kupata Daraja la ufaulu.
Kimsingi, kila somo lilikuwa na NMD yake kulingana na
Continued Assessment (
CA) zilivyo kwa mwaka husika. Lakini mwaka 2012 Baraza lilitumia Mfumo Mpya ambao ulikuwa haubadiliki kutegemea hali ya ufaulu wa Mwanafunzi, yaani kuwa na Viwango Maalum vya Kutunuku (
Fixed Grade Ranges
).
Tume imebaini kwamba, pamoja na kwamba Mfumo huo uliandaliwa kwa nia nzuri,Utaratibu huo mpya haukufanyiwa utafiti na maandalizi ya kutosha kabla ya kutumika.
MAPENDEKEZO YA AWALI YA TUME
7.
Mheshimiwa Spika,
kwa kuzingatia masuala mbalimbali yaliyojitokezawakati wa uchunguzi, Tume katika Taarifa yake ya awali imetoa mapendekezo mbalimbali yakiwemo yale yanayohitaji kutekelezwa kwa haraka.
Kutokana na kuwepo kwa mapendekezo hayo ambayo inabidi yafanyike kwa haraka, tarehe 29 Aprili, 2013 Baraza la Mawaziri lilipokea Taarifa ya Awali ya Tume na kuijadili ambapo liliridhia mapendekezo hayo yaanze kutekelezwa mara moja.
Maamuzi hayo ya Baraza la Mawaziri yanalenga kutenda haki kwa Walimu na Wanafunzi ambao juhudi zao za kufundisha na kujifunza zimepimwa kwa kutumia Mfumo mpya ambao hawakupata fursa ya kushirikishwa na kuandaliwa.
Mapendekezo hayo niyafuatayo
:i.Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012
yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011
;
ii.
Standardisation
ifanyike ili matokeo ya Wanafunzi yalingane na juhudi walizoziweka katika kusoma kwa mazingira na hali halisi ya Tanzania na uamuzi wa Taifa kuongeza idadi ya Shule naWanafunzi wakati uwekezaji katika ubora unaendelea;
iii.Baraza la Taifa la Mitihani limeelekezwa kuzingatia kuwa pamoja na kwamba Sheria ya kuanzishwa kwake inawaruhusu kufanya marekebisho ya mchakato wa mitihani, lakini marekebisho yoyoteya kubadilisha Utaratibu wa kupanga viwango vya ufaulu na madaraja ya matokeo ya Mitihani,
lazima yahusishe Wadau wote wanaohusika na Mitaala, Ufundishaji na Mitihani
.
Wakati Tume inaendelea kukamilisha kazi yake, uamuzi wa Baraza la Taifa la Mitihani wa kutumia utaratibu mpya wa kupanga viwango vya ufaulu na madaraja ya matokeo ya Mitihani
uliotumika mwaka 2012 usitishwe
na badala yake Baraza la Mitihani litumie
Utaratibu wa mwaka 2011 kwa Kidato cha Nne na cha Sita kwa Mitihani yote ukiwemo utaratibu wa
Standardization
na kutoa Matokeo mapya kwa kuzingatia maelekezo haya.
Aidha, mchakato wa Mfumo wa Tuzo wa Taifa (
NationalQualifications Framework
) na Mfumo wa kutahiniwa/kutathmini maendeleo ya Mwanafunzi katika masomo yake (
National Assessment Framework
) ukamilishwe haraka iwezekanavyo.
5
UTEKELEZAJI WA MAPENDEKEZO YA TUME
8.
Mheshimiwa Spika,
kutokana na umuhimu wa mapendekezo hayo,Baraza la Mawaziri limeamua kwamba utekelezaji wa mapendekezo hayouanze mara moja.
9.
Mheshimiwa Spika,
Tume ya Uchunguzi itaendelea kukamilisha Taarifa yake vizuri kwa kuhusisha Wadau mbalimbali ili kupata maoni zaidi naushauri wao juu ya mambo mbalimbali yaliyobainika wakati wa uchunguzikabla ya kuikamilisha na kuitoa kwa matumizi ya Umma na Vyombombalimbali.
HITIMISHO
10.
Mheshimiwa Spika,
Serikali inaipongeza sana Tume kwa kutoa mapendekezo ya awali ambayo Serikali imeyaridhia.
Aidha, Serikali inawashukuru Wananchi wote na Wadau mbalimbali wa Sekta ya Elimu wanaoendelea kutoa maoni na ushauri wao kwa Tume.
11.
Mheshimiwa Spika,
Serikali inawahakikishia Wananchi kuwaitaendelea kuboresha Elimu Nchini ili kuwezesha Watoto wetu wapate mafanikio katika maisha na maendeleo yao, kwani Wahenga wanasema
“Elimu ni Ufunguo wa Maisha”
.12.
Mheshimiwa Spika,
naomba kuwasilisha.
HILI BARAZA JAMANI MBONA MNALIONEA HAYA AU NDO MFUMO KRISTO WAISLAMU WAMETOA MAONI YAO MAPEMA KABISA BARAZA LIREKEBISHWE MNANG'ANG'ANIA. MATOKEO MABAYA YALITOLEWA MAKSUDI ILI BARAZA LIJISAFISHE KWA KITENDO CHAKE KILICHOFANYA MWAKA 2011 KUWAFUTIA MATOKEO WANAFUNZI WASIO NA HATIA HUSUSAN WAISLAM NA WAZANZIBARI LAKINI MUNGU HAMFICHI MNAFIKI MAMBO BADO.......
ReplyDeletehizi data si za kweli mnajidanganya tu
ReplyDelete