Habari za Punde

TRA yasaini mkataba na kampuni 11 kusambaza mashine za EFDs

Na Fatuma Kitima,DSM
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeingia makubaliano ya mkataba na kampuni 11 ambazo zitafanya kazi ya usambazaji mashine,kufundisha watumiaji na kutoa huduma ya matengenezo kwa wakatipale zinapoharibika.

Taarifa hiyo ilitolewa Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya utekelezaji wa mradi wa mashine za kielektroniki.

Naibu Kamishna Mkuu (TRA) Rished Bade alisema kampuni zilizoingia mkataba ni Advatech Offices Sulutions Ltd,Busness Mashines Tanzania Ltd,Bolsto Solutions Ltd,Checknocrats Ltd, Compulynks Ltd, Maxcom Afrika Ltd,Pergamon Tanzania Ltd, Powercomputers na Telecommunication Ltd, SoftNet Technologies Ltd,Total Fiscal Solutions na Web Teknologies Ltd.


Bade alisema mbali na kampuni hizo kufanya kazi ya usambazaji wa mashine pia kuna kampuni nne zitasambaza karatasi zenye ubora wa kutoa risiti zisizofutika.

Alitaja kampuni hizo kuwa ni Advatech Office Solutions Ltd, Business Machines Tanzania Ltd,Checknocrats Ltd na Total Fiscal Solution Ltd.

Aidha alisema wasambazaji wataendelea kutoa elimu kwa makundi mbalimbali.

Naye Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Maxmalipo (COO) Ahmed Lussasi amewaomba wafanyakazi kuchukua mashine hizo kutoka Max kwa kuwa iwapo itaharibika itatengenezwa kwa haraka.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.