Habari za Punde

Boti Mpya ya Kampuni ya Azam Marine Kilimanjaro 4 Yaanza Safari Zake .

 Boti mpya ya Kilimanjaro 4 ikiwasili katika bandari ya Zanzibar ikitokea Dar-es-Salaam baada ya kuanza kutowa huduma ya usafiri kwa pande hizo mbili na kurahisisha usafiri kati ya Dar na Zenj kuwa wa uhakika zaidi kwa kuongezeka kwa vyombo vya usafiri Zanzibar.
 
Na kupunguza ulanguzi wa tiketi kwa abiria wakati wanapotaka kusafiri kukosa boti kwa kisingizio cha boti chache na hatimai kuuzwa tiketi hadi shilingi Elfu thelathini. 
 
Ujio wa boti hii utapunguza tatizo hilo kwa maana huchukua abiria 700 kwa wakati mmoja

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.