Habari za Punde

Tanzania yaweka historia yatia sahihi mkataba wa biashara ya Silaha

Picture
Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akitia sahihi kwa niaba ya Serikali,Mkataba wa Kimataifa wa Kudhibiti Biashara ya Silaha ( ATT) Tanzania ilikuwa kati ya nchi 67 za kwanza ambazo zimetia sahihi katika siku ya kwanza ya uzinduzi wa tukio hilo la kihistoria.
 
Baada ya Mkataba kutiwa sahihi nchi zaidi ya 50 kama sheria zinavyotaka utaanza kufanya kazi rasmi baada ya siku 90. Mkataba huu ambazo umechukua zaidi ya miaka sita hadi kupatikana unalenga katika pamoja na mambo mengine kusimamia na kuratibu biashara ya silaha zikiwamo mizinga ya kivita, magari ya deraya, ndege za kivita, helkopta za mashambulizi, meli za kivita na silaha ndogo na nyepesi.
 
Vile vile mkataba unalenga kudhibiti silaha zisiangukie mikononi mwa makundi ya kihalifu yakiwamo ya kigaidi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.