Habari za Punde

Msajili w Vyama vya Siasa Aapishwa

Na Mwandishi wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete jana alimwapisha Jaji Francis Sales Katabazi Mutungi kuwa Msajili mpya wa vyama vya siasa.

Jaji Mutungi anachukua nafasi ya John Tendwa ambaye amestaafu utumishi wa umma kwa mujibu wa sheria.

Sherehe za kumwapisha Jaji Mutungi zilizofanyika Ikulu, Dar es Salaam zilihudhuriwa pia na Jaji Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman, Jaji Kiongozi, Fakhi Abdallah Rheno Jundu na Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.



No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.