6/recent/ticker-posts

Sultan Qaboos Aipa Zanzibar 12bn/-. 16 Wadhaminiwa na Masomo ya Juu Kupitia Qaboos Fund.

Na Kassim Ali, Amina Abeid, ZJMMC
SULTAN Qaboos bin Said wa Oman ametoa msaada wa riali 3,100,000 (zaidi ya shilingi bilioni 12.669) kwa ajili ya ujenzi wa msikiti mkubwa wa kisasa katika eneo la Chuo cha Kiislamu Mazizini nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mazizini,Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Ali Juma Shamhuna alisema ujenzi wa msikiti huo unatarajiwa kuanza wakati wowote baada ya kutiwa saini makubaliano ya msingi kati ya Zanzibar na Oman.

Alisema msikiti huo, pamoja na shughuli za ibada, pia utakuwa ni chimbuko la kuanzishwa Chuo Kikuu cha Kiislamu Zanzibar na kufanikisha azma ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Abeid Amani Karume aliependekeza kujengwa Chuo Kikuu cha Kiislamu katika eneo hilo wakati akikifungua chuo hicho.

“Maandalizi yote ya ujenzi msikiti huu yamekamilika na utakuwa na sehemu ya kusalia wanawake na wanaume, madarasa sita ya kusomea, chumba cha kompyuta na maktaba ya kisasa,” alisema.

Akizungumzia msaada wa masomo ya elimu ya juu uliotolewa na Mfalme Qaboos kupitia mfuko wa Sultan Qaboos Academic Fellowship, alisema umeanza kuleta mafanikio na wanafunzi wa kwanza 16 wataanza kufaidika na msaada huo mwaka huu.

Alisema wanafunzi tisa watasoma shahada ya uzamivu (PhD) na saba watachukua shahada ya uzamili katika fani walizoomba na watajiunga kwenye vyuo vikuu vya nchi tofauti duniani.

Aliongeza kuwa awali Wazanzibari 170 walipeleka maombi ya kupatiwa nafasi hizo kupitia mtandao na baada ya mchakato uliofanywa na kamati mbili zilizoundwa kushughulikia maombi hayo, waliobahatika ni watu 16.

Waziri Shamuhuna aliwatoa wasi wasi wananchi kuwa hakukuwa na upendeleo wa aina yoyote katika kuwapata wanafunzi hao na kila kitu kilifanywa kwa njia ya mtandao.

“Tumekataa suala la ujomba au ushangazi katika nafasi hizi, tumetumia mtandao kuwapata wanafunzi bora na hao ndio waliofaulu kutokana na masomo waliyoomba na sifa walizanazo,”alisema.

Alisema hivi sasa wanaendelea kuboresha masomo ya sekondari na hivi karibuni watakwenda Oman kuzungumzia suala hilo ili kupata wanafunzi wengi zaidi wenye sifa za kujiunga kupitia msaada wa Sultan Qaboos.

Post a Comment

3 Comments

  1. Hizo bilioni 12 ndio zote zilizotolewa au watanganyika washachukua zao hapo?

    ReplyDelete
  2. Natamani Bln. 12 hizi zingetumika kukibadili kile chuo cha afya Mbweni kuwa chuo kishiriki cha SUZA na kuanza kutoa Degree za AFYA

    Uongozi wa SMZ unatakiwa pia kutumia msaada huu kwa kuandaa wanafunzi wa sayansi pale LUMUMBA SCHOOL ili wazitumie fursa hizi vizuri.

    Tutafanya kosa la kihistoria kama tutatumia msaada huu, kwenda kusomesha watu PhD za masomo ya SANAA (arts) halafu tuseme hatumna madaktari bingwa.

    "Uso umeumbwa na haya" wenzetu wameamua kulipa fadhila, baada ya muda mrefu wa kusahau historia.

    Tukishindwa kuitimia fursa hii vizuri, tutakuja kuishia yale ya miaka ya 60 na 70 wakati Z'bar ilipokua na uwezo, kln. badala ya Serikali kutumia vizuri rasilimali wakaamua kufuja.

    ReplyDelete
  3. Nibora wazichuke hao watanganyika,kuliko hawa smz, mijtu isio rikra, dunia ya leo znz, hakuna watu wano swali nje,baadayakuomba misaada ya kujenga vyuo vya ufundi watoto wo wapate kuingia kwenye soko la ajira, wao na muamsho kakilizao sawa, wazanzibar hatuna pakushika

    ReplyDelete