Habari za Punde

Padri mwengine amwagiwa tindikali


Padri wa kanisa Katoliki Parokia ya Cheju Zanzibar, Anselmo Mwangamba amejeruhiwa usoni na kifuani baada ya kumwagiwa tindikali na Watu wasiojulikana katika maeneo ya mlandege jioni ya leo, akiwa katika harakati zake kupata habai na kuwasaliana na jamaa kupitia mtandao wa Internet katika Cafe ya Sunshine mlandege, kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walisikia Padre hiyo akilalama kuwa amamwagiwa kitu cha majimaji na kuomba msaada kwa wananchi wa eneo hilo, na kupata msaada wa huduma ya kwanza kutoka kwa mfanyakazi wa Cafe hiyo kwa kutowa maji baridi na kumwagiwa. kwa mujibu wa dada wa duka hilo Padre huyu hufika hapo kila siku kupata huduma ya internet. Mkasa huo umemfika baada ya kumalizi kupata huduma hiyo na kutoka nje akiwa katika eneo hilo walitokea watu wasiojulikana na kumwagia kitu hicho kinachodhaniwa na tindi kali.

1 comment:

  1. vijana wa uvccm tayari wanaanza tena vitimbi vyao, ili kukoroga mpango wa mabadiliko ya katiba ya kudai Zanzibar huru na kuifanya Zanzibar ionekane kuna udini.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.