6/recent/ticker-posts

Warioba Katiba Haipatikani kwa Maoni ya Upande Mmoja.

Warioba:Katiba haipatikani kwa maoni ya upande mmoja


Na Mwandishi wetu, DSM

MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, ameonya kwamba hakuna katiba itakayopatikana kwa kusikiliza maoni ya upande mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Jaji Warioba aliyashauri makundi ya kisiasa yanayovutana yakutane kujadili kwa kina suala hilo na hatimae kufikia muafaka.

Alisema Watanzania wanahitaji katiba bora itakayohusisha mawazo ya makundi yote, hivyo wanasiasa wanapaswa kutafakari kwa pamoja badala ya kugawanyika.

Alisema huu si wakati wa kuvutana na malumbano badala yake ni wa kutafakari na kushauriana kwa pamoja ili Tanzania ipate katiba bora.

“Tunataka katiba bora itakayoridhiwa na Watanzania wote na sio kuanzisha malumbano yasiyo na msingi,” alisema.

Hata hivyo, alisema Tume itaridhia marekebisho ya sheria mabadiliko ya katiba yaliyopitiwa na Bunge baada ya kusainiwa na Rais.

Post a Comment

0 Comments