Balozi Seif akiuhutubia umati mkubwa wa wanachama wa Klabu ya Kimataifa ya Rotary Mjini Seattle katika hafla ya chakula cha mchana kuwakaribisha viongozi wapya na kuwaaga wale wa zamani wa Klabu hiyo.
Mtaalamu wa masuala ya maabara ya afya ya Taasisi ya Kimataifa ya Misaada ya Path Bwana Glenn Austin akitoa ufafanuzi wa kazi za Taasisi hiyo kwa Balozi Seif na Ujumbe wake walipotembelea ofisi za Taasisi hiyo zilizopo kati kati ya Mji wa Seattle – Washington.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Mkurugenzi wa Taasisi ya kimataifa inayotoa huduma za Afya ya Path Mjini Seattle Bibi Ellen Cole mara baada ya kutembelea Osifi za Taasisi hiyo yeye na ujumbe wake.
Mtaalamu wa masuala ya afya wa Taasisi ya Path Bibi Tula De los Santos akiutembeza ujumbe wa Zanzibar unaoongozwa na Bakamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ndani ya jengo la Taasisi hiyo liliopo Mjini Seattle.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Klabu ya Kimataifa ya Rotary ya Seattle Nchini Marekani Bibi Laure Rehrmann kushoto yake pamoja na Mjumbe wa Rotarry Bwana Ferouzi Sefrioui.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi na Ujumbe wake wakijumuika pamoja na wanachama wa Klabu ya Kimataifa ya Rotary ya Mji wa Seattle katika tafrija nya kuwakaribisha viongozi wapya na kuwaaga wale wa zamani wa Klabu hiyo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja yeye na ujumbe wake pamoja na Uongozi wa Taasisi inayotoa midaada ya kiafya ya Path Mjini Seattle.
No comments:
Post a Comment