Na Mwajuma Juma.
KIKOSI cha timu ya Taifa ya Zanzibar ya mpira wa Kikapu kinachoundwa
na wachezaji 26 kimetangazwa ambacho kitashiriki michuano ya mchezo
huo ya Kombe la Mapinduzi yatakayoanza Januari 8 mwakani.
Kocha Mkuu wa timu hiyo Mzee Haji Jecha amesema kuwa kikosi hicho
baadae kitafanyiwa mchujo na kubakishwa wachezaji 15.
Aliwataja wachezaji hao kuwa ni Ramadhan Amour, Abdulhakim Khamis,
Yahaya Anania, na Abdalla Riziki (JKU), Abdulfalah Mohammed, John
Fanuel, Gimakisa Alfonce, Godfrey Christopher na Amani Kitomari
(Nyuki).
Wengine ni Amiri Muhidini, Mohammed Kassim, Said Ali na Saleh Abass
(Polisi), Mohammed Asaa, Mohammed Bakari, Hussein Said na Abass Juma
(Rangers), Said Kassim, Haji Hamad na Fowadi Mohammed (Stone Town).
Aidha alisema kuwa katika timu hiyo amechaguwa na wachezaji vijana
ambao watasaidia kuliongoza gurudumu la timu hiyo
Wachezaji vijana ni Abdulwahidi Khamis (Polisi), Yussuf Abdi (African
Magic), Amri Sharif (Spider), Said Masoud (Raptors) Nassor Salum (New
West) na John Oscer (Rangers).
Hata hivyo akizungumzia kuanza kwa mazoezi alisema bado hajajua
ataanza lini hadi pale uongozi wa chama mchezo huo Taifa utakapowaita
na kutaja siku ya kuanza kwa mazoezi.