Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS DKT.BILAL Aendesha Zoezi la Harambee ya Kuchangia Madawati Mfuko wa Maendeleo ya Elimu JIMBO la Nkenge

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal Fabian Masawe
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti, Mkurugeniz wa Kagera Sugar, Hamadi Yahya, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake wa kuchangia maendeleo ya Elimu ya Jimbo la Nkenge mkoa wa Kagera,wakati wa hafla ya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Elimu Jimbo la Nkenge kununua madawati ili kusadia shule za msingi za Jimbo hilo. Harambee hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam, jana usiku. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Asumta Mshana na (kushoto kwa Makamu) ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanal Fabian Masawe
Meza Kuu wakijumuika kuimba wimbo maalumu wa mkoa wa Kagera wa kuhamasisha maendeleo ya mkoa huo, hususan katika suala la elimu na kuchangia madawati.

  Mbunge wa Jimbo la Nkenge, ambaye ni mratibu wa Harambee hiyo, Asumta Mshana, akizungumza kutoa ushuhuda wa matatizo ya Elimu katika jimbo lake
 Msanii wa Sanaa ya Ngoma akitumbuiza katika hafla hiyo ya harambee ya kuchangia madawati kwa skuli za Jimbo la Nkenge. Picha na OMR




2 comments:

  1. mheshimiwa hongera kwa jitihada zako, lakini nina suala 1 tokea uingie madarakani ulijaaliwa kuwafanyia chochote zanzibar?, au nitakua naleta uchochezi?

    ReplyDelete
  2. Na mimi nililuwa na suala hill hilo

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.