Nyumba hii ni moja ya matunda ya Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964, ambayo ilijengwa mwaka 1935 katika mji wa Chake Chake Pemba, ambayo Serikali kwa makusudi iliwapatia Wananchi kwa ajili ya Makaazi.
Lakini wakaazi wa Nyumba hii hawajaona umuhimu wa kuifanyia hata matengenezo angalau kuthamini juhudi za Serikali yao , maendeleo kama hayo nayo isubiriwe Serikali kwa mara nyengine iwafanyie matengenezo ndio ujuilikane inawajali Wananchi ?.
Ni vyema waliopewa majumba kama haya kuwa na utamaduni wa kuyafanyia matengenezo japo kwa rangi ili kuthamini juhudi za Serikali yao.
Picha na Maelezo na Bakar Mussa, Pemba
tulio wengi tunasubiri kiharibike halafu tuilalamikie serikali hatuwezi kujifanyia hata mambo madogo madogo wenyewe lawama zote inatumiwa serikal hasa hii ya ccm labda wengi wetu tunaona mapinduzi yalikua sio halali sasa sio vizuri kula matunda yake
ReplyDeleteMbona ammmy waonyesha una ajenda yako? Hivi umeona ni wakaazi wa nyumba hii tu wameshindwa kuyathamini matunda ya Mapinduzi kuwa hawajaikarati nyumba iliyojengwa Mwaka 1935 na ndio ikawa matunda ya Mapinduzi ya 1964 (makubwa hayo)?
ReplyDeleteMbona husemi zile nyumba zilizo matunda ya Mapinduzi za mwaka 1972 (Michenzani), za mwaka 1979 (zipo nyingi sana twaziita nyumba za vijiji sera ya Mh Jumbe?). Kunaiona nyumba ya Chake tu ambayo wala hatukuijenga sisi wana wa Mapinduzi?
ndugu yangu bakar mussa jina lako zuri lakini kidogo umekosea , hayo mapinduzi uliyaona mpaka ukayapa utukufu? hakuna utukufu ila kwa Mola pekee , laiti ungejua madhumuni ya mapinduzi usingeyaita matukufu , yatatumaliza sisi na vizazi vyetu , ukija kushtuka utakuwa umechelewa, naomba katafute historia ya kweli sio ilioandikwa na wanasiasa , wewe si mwandishi wa habari? kwanini usitembee kuwatafuta watu waliokuwa hai wakati ule ukawauliza ukweli ?
ReplyDeleteSerikali ya MAPINDUZI ilipora tu hiyo nyumba kwa mwenyewe ndio maana iko hivyo kwa kuwa si mporaji wala hao wakaazi ambao wana uchungu nayo.
ReplyDeletekumbe hawa kina maalim seif na wenzake wanapo yatetea mapinduzi na kusema mzee karume kua yuko sawa hawajui kitu au ni kuwatia watu changa la macho tu ili wakubalike kazi ipo zanzibar
ReplyDeletewanaotetea mapinduzi kina dr sheni mbona huwataji , na hujiita kwa majivuno mwenyekiti wa baraza la mauaji , duh ! nimekosea mapinduzi
ReplyDeleteKuna Mh mmoja wa CUF ambae analani mapinduzi kwa nguvu zote ila '' inayoitwa zulma ya mapindizi anaing'ang'ania''. Ni hivi ama aliwekwa au alijiweka katika jumba la waliokimbia mapinduzi ya 1964. Sasa wenyewe hivi karibuni walijitokeza kuja kudai HAKI YAO. Mh huyu kamaliza ngazi zote za sharia na ameshindwa kuibadilisha HAKI kuwa BATILI. Matokeo kang'oa tiles alotia. Huyu ni damu yangu na imetuathiri kuipoteza nyumba ile kwasababu ndio nyumba kuu katika family. Kwahio Sidhani kama kuna wakweli kwenye matunda ama dhuluma ya Mapinduzi.
ReplyDeleteNinavyoelewa mimi hili ni mojawapo kati ya majumba ya C.P. JANNI (kiongozi wa dini ya kihindu) aliyeletwa Z'bar kutoka India, jengo lake jengine (rangi ya kijani) lipo Unguja nyuma ya Beti la jaibu kwenye kona ya kupandisha mtaa wa Hurumzi.
ReplyDeleteLengo la mtawa huyo wa kihindu ilikua ni uwekezaji. na baada ya mapinduzi majengo hayo yalitaifishwa na Serikali. na kukodishwa kwa wananchi wakiwemo wafanyakazi wa serikali.
Kwa uwelewa wangu mdogo wa sharia ya Ardhi ,ktk kipengele cha upangishaji (leases) ni kwamba mmiliki au 'Landlord' ambapo kwa hapa ni SMZ ndiye mwenye dhamana ya kufanya matengenezo kwa vile wapangaji wanalipa kodi!
Majengo ya namna hii yapo mengi Z'bar likiwemo lile la 'treni' pale Darajani ambalo lina wapangaji wa nyumba na maduka na wote wanalipa kodi lkn. wallahi SMZ hawajawahi kulipiga hata chokaa pamoja na kuwa kwenye uso wa mji!
No research, no right to speak' mzee wangu mmoja sasa marehemu aliwahi kuishi ktk jingo la C.P. JANNI chake-chake akiwa karani wa mahkama na shangazi wa mke wangu hadi leo hii anaishi ktk jengo la C.P. JANNI hurumzi. historia ya C.P. JANNI niliipata kutoka kwa baniani mmoja aitwae KIMJI ambae ni dobi maarufu hapa Z'bar na anaishi Vuga na hupendelea kuanika nguo zake pale MNAZI MMOJA.(mbele ya skuli ya Ben bella)..tuache kukurupuka!