ZAIDI ya watu 400,000 wapo hatarini kupata ugonjwa wa Kisukari
viswiwani Zanzibar.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Dkt. Sira Ubwa
Mamboya alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika
kuadhimisha siku ya Kisukari Dunaini huko ofisini kwake Vuga mjini
Zanzibar.
Alisema kuwa Zanzibar hivi sasa ina watu zaidi ya 400,000 wenye uzito
mkubwa ambao ni moja kati ya viashirio vya kupata kwa ugonjwa huo.
Hata hivyo alisema kuwa kuongezeka kwa ugonjwa wa kisukari katika nchi
nyingi kunatokana na kupanuka kwa miji pamoja na kasi ya maendeleo
ambao hupelekea kubadili mfumo wa maisha ikiwa ni pamoja na mabadiliko
ya kijamii na kiutamaduni, kutofanya mazoezi, ukosefu wa lishe bora na
matumizi ya tumbaku na pombe.
Hivyo alisema kuwa kutokana na hali hiyo wanahitaji kuwa waangalifu
nayo ili kuzinusuru afya zao na kusema kuwa ni muhimu kwa wananchi
kujikita katika mazoezi na kuacha visingizio vya kukosa muda.