Tegemeo la CCM ni Amani na Utulivu-Thuwaiba


Na Mwajuma Juma, Zanzibar

MWAKILISHI wa Jimbo la   Fuoni Bi Thuwaiba Edington Kisasi amesema kuwa tegemeo la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni amani na utulivu na bila ya CCM vitu hivyo havitakuwepo.



Bi Kisasi alitoa tamko hilo jana  katika uzinduzi wa Jengo la Biashara la UVCCM Zanzibar liliopo Darajani wilaya ya Mjini Unguja.

Alisema  kuwa CCM ndio chama pekee ambacho kinajali kuwepo kwa amani jambo ambalo limekuwa kizingatiwa na Serikali za nchi mbali mbali.


Alisema kuwa hakuna Serikali hata moja ambayo itataka kuona wananchi wake wanaishi katika mazingira yasiyoridhika yakiwemo ya vurugu hasa kwa  vijana wake.



Hivyo aliwataka vijana kukubaliana na matakwa ya viongozi wao hasa kwa yale mambo ambayo yanafaida kwao na taifa kwa ujumla.



Mapema Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Bw. Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa kuimarika kwa vitega uchumi vya Jumuiya yao ni kuimarika kwa uchumi wa CCM, hivyo alisema kuwa  UVCCM inampango wa kuimarisha vitega uchumi vyake vyote ili kuiendeleza Jumuiya yake pamoja na CCM kwa ujumla.



Akizungumza katika hafla hiyo Mkurgenzi wa Kampuni ya Mshely Clearing & Forwarding Limited iliyosimamia ujenzi wa jengo hilo Bw. Ramadhan Simai Makame amesema kuwa jumla ya shilingi bilioni 2.2 zimetumika
hadi kukamilika kwake, ambapo Kampuni hiyo imetiliana mkataba wa miaka 30 na UVCCM ambapo kupitia mkataba huo UVCCM watapata asilimia 30 na asilimia 70.

Post a Comment

Previous Post Next Post