Habari za Punde

Kongamano la Bunge la Vijana Zanzibar kutimia miaka 50 ya Mapinduzi Zanzibar.


 Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Ali Abdalla Ali akihutubia wakati wa ufunguzi wa Bunge la Vijana Zanzibar, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani Kikwajuni Zanzibar.
 Katibu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Yahya Khamis Hamad, akitowa maelezo ya Kongamano la Bunge la Vijana Zanzibar wakati wa ufunguzi wa kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Baraza wa Zamani Kikwajuni Zanzibar.

 Mhe. Spika akifuatilia michango ya Wabunge wakati wa kuchangia hutuba ya Serekali kuhusiana maendeleo ya Vijana 
                                   Mdau kutoka jumuiya ya Wasioona akichangia katika bunge hilo
 Mheshimiwa mbunge akichangia katika kikao hicho kuhusiana na maendeleo ya Vijana, wakati wa kuchangia Taarifa ya Serekali kuhusiana na Vijana. 

 Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Ali Abdalla Ali akifuatilia michango ya Wabunge wa Bunge la Vijana 
                               Waheshimiwa Wabunge wakifuatilia michango ya Wabunge wakiwasilisha 
Waziri wa Uwezeshaji Uatawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Mhe. Shaaban Ali Abdalla, akijibu michango ya Wabunge waliowasilisha katika Bunge hilo la Vijana, lililofanyika katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Zanzibar.  
Waheshimia Wabunge wakimsikiliza Wazri wa Uwezeshaji akijibu michango ya Wabunge waliowakilisha katika Bunge hilo lililowajumuisha Vijana kutoka Wilaya za Unguja na Pemba 
Spika akitoka katika ukumbi wa mkutano baada ya kuahirisha Bunge la Vijana, ikiwa ni kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar, lililofanyika katika ykumbi wa Baraza la Wawakilishi wa Zamani kikwajuni.
 Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Ali Abdalla Ali akiwa katika picha ya pamoja na  Bunge la Vijana na Mawaziri .baada ya Kikao chao cha Bunge la Vijana kuzungumzia Maendeleo ya Vijana kwa Ujumla na Mafanikio yao katika sekta mbalimbali za maendeleo.  
 Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Ali Abdalla Ali akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Bunge la Vijana na Mawaziri .baada ya Kikao chao cha Bunge la Vijana kuzungumzia Maendeleo ya Vijana kwa Ujumla na Mafanikio yao katika sekta mbalimbali za maendeleo. 1 comment:

  1. Ajabu ya hili bunge lavijana, niwalewale, watoto wa viongozi hakuna makundi ya watoto wa wakulima na wakwezi, ndio tutafika kweli? tungefurahi kama utwawekwa utaratibu maluma ya kuwapata hao wabunge wa vijana, tusikurupuke kuiga nahali tumeja ubinapsi na chuki

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.