Habari za Punde

Maalim Seif akagua maendeleo ya uwekaji nyasi bandia uwanja wa Amaan


Na Hassan Hamad OMKR

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ametembelea uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar kukagua maendeleo ya zoezi la uwekaji wa nyasi bandia katika uwanja huo.

Meneja wa uwanja huo Khamis Ali Mzee, amesema zoezi hilo linaendelea vizuri, huku wakiendelea kukusanya vifaa zaidi kwa ajili ya kukamilisha zoezi hilo kwa wakati muafaka.

Amesema vifaa vinavyoendelea kukusanywa kwa sasa ni pamoja na mchanga maalum ambao unakwenda sambamba na uwekaji wa nyasi hizo ili kuweka umadhubuti zaidi wa uwanja huo.

Kwa upande wake mkandarasi wa uwekaji wa nyasi hizo bw. Ben Mushi kutoka kampuni ya EKIKA ya Dar es Salaam, amesema mvua zinazoendelea kunyesha  zinazorotesha zoezi hilo.

Hata hivyo amesema watafanya kila juhudi kuona kuwa zoezi hilo linakamilika kwa wakati, ili uwanja huo uweze kutumika kwa sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi, zinazotarajiwa kufika kilele chake tarehe 12 Januari, 2014.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.