WAKE waWawakilishi na Wabunge wakifuatilia hutuba ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, kwa Wajasiriamali Wanawake wa Vikundi vya Ushirika vya Mkoa wa Kaskazini Pemba.katika ukumbi wa Jamuhuri Wete.
MKE wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Balozi akitowa nasaha zake kwa Vikundi vya Ushirika vya Wajasiriamali Wanawake vya Mkoa wa Kaskazini Pemba wakati wa Ziara ya Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Ujumbe wake wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge kutowa michango yao kwa Vikundi hivyo.
WANAWAKE wa Vikundi vya Ushirika wakimsikiliza Mke wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akiwahutubia na kutowa nasaha zake wakati wa ziara yake kutembelea vikundi hivyo na kutowa msaada wa nyezo za kufanyia kazi
MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Kaskazini Pemba Bi. Saada Thani akizungumza katika mkutao huo na kutowa maelezo ya maendeleo ya vikundi vya Wanawake Wajasiriamali katika mkoa wake.
MKE wa Balozi Mdogo wa China aliopo Zanzibar Bi Wu Yan akiwasalimia Wanawake Wajasiriamali wa Mkoa wa Kaskazini Pemba wakatika wa ziara ya Mama Mwanamwema Shein kutembelea Vikundi hivyo.
No comments:
Post a Comment