Habari za Punde

Balozi Seif akutana Ujumbe wa sekta ya wawekezaji kutoka Italia

 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na wawekezaji wa sekta tofauti za Kiuchumi kutoka Nchini Italy Hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar kulia yake ni kiongozi wa Ujumbe Huo Profesa Martin Antonio Morina


Na Othman Khamis Ame, OMPR

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  alikutana kwa mazungumzo na ujumbe wa Wawekezaji  wa Sekta tofauti ya kiuchumi kutoka Nchini Italy ambao upo Zanzibar kuangalia mazingira ya jinsi watakavyoweza kuwekeza vitega uchumi vyao.

Katika mazungumzo yao yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Vuga Mjini Zanzibar Kiongozi wa Ujumbe huo Rais wa Chama cha Mchezo wa Karati Duniani Profesa Martin Antonio Morina  alisema ujumbe huo umevutiwa na mazingira mazuri yaliyopo ndani ya Visiwa vya Zanzibar jambo ambalo limewapa ushawishi wa kutaka kushirikiana na Zanzibar katika  Sekta ya uwekezaji.

Profesa Martin Antonio alimueleza Balozi Seif kwamba ujumbe wake uko katika harakati za kuonana na Taasisi husika za uwekezaji hapa Zanzibar katika kuona  wanaweza kuwekeza katika ujenzi wa Kituo cha Michezo { Sports Academy }, Huduma za Afya katika Sekta ya Utalii pamoja na suala la Umeme wa jua.

Alisema Wafadhili na wataalamu wa sekta hizo tatu tayari wameshaonyea niya ya kutaka kuanzia miradi hiyo ili isaidie kuinua sekta ya Utalii ambayo inaonekana kupewa msukumo mkubwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar sambamba na kutoa ajira kwa Wananchi wazalendo.


Akitoa  shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar 
Balozi Seif Ali Iddi aliueleza ujumbe wa wawekezaji hao kutoka Nchini Italy kwamba Zanzibar  imeacha milango wazi kipindi kirefu sasa kwa kukaribisha wawekezaji wa Kigeni kusaidia miradi ya kiuchumi hapa Nchini.

Balozi Seif alielezea faraja yake kutokana na nia ya wawekezaji hao kutaka kuwekeza miradi yao ambayo kwa kiasi kikubwa ile waliyoipendekeza  imekuwa na umuhimu mkubwa kwa wananchi wa Zanzibar hasa katika kipindi hichi cha mabadiliko ya sayansi na Teknolojia Duniani.

“ Sekta zote mlizoainisha kutaka kuzitekeleza hapa Nchini ambazo ni Ujenzi wa Kituo cha Michezo, Hudumza za Umeme pamoja na huduma za afya katika Sekta ya Utalii ni muhimu “. Alisema Balozi Seif.

Ujumbe huo wawekezaji kutoka Nchini Italy umebeba wataalamu wa nawekezaji kutoka katika sekta za Michezo mbali mbali , Nishati, huduma za  Afya pamoja na Utalii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.