Na PascalBuyaga, Tarime
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini IGP, Arnest Mangu, ametuma timu ya
wapelelezi wilayani Tarime, kumsaka na kumkamata mtu anatekeleza mauaji na
kisha kutokomea porini.
Mtu huyo aseiejulikana amekuwa akitumia risasi kufanya mauaji ambapo
watu wanane wameshauawa katika kipindi cha siku tatu.
Mtu huyo amekuwa tishio la wakazi kwa wakazi wa wilaya hiyo hali
iliyosababisha baadhi ya watu kulazimika kusitisha shughuli zao kiuchumi.
Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Tarime, Marco Nega, alisema tangu
Januari 27 hadi sasa hospitali hiyo imepokea watu wanane waliouawa kwa risasi.
Alisema usiku wa Januari 27 mtu anayedaiwa kufanya matukio hayo
alimuua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Juma Marwa dereva wa bodaboda mkazi
wa Nkende wakati akiwa njiani kuelekea nyumbani kwake.
Alisema aliendelea kupokea maiti za watu wengine saba akiwemo
mwanajeshi mstaafu, Zachalia Mwita (58) tangu mauaji hayo yalipoanza Januari
26.
Katika matukio mengine mtu huyo anadaiwa kuwajeruhi kwa risasi watu
watano ambao ni Mgosi Marwa na Juma Mwita wakazi wa Mogabiri,Joseph Richard na
Gastor Richard wakazi wa Rebu pamoja na mhandisi wa ujenzi Mwasi Yomani ambao
kati yao wawili inadaiwa tayari wameshafariki.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na matukio hayo, mkazi
mmoja wa Tarime, Wambura Marwa, alisema wameshutushwa na hali iliyotokea na
kuviomba vyombo vya dola kuhakikisha mtu huyo anakamatwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa
Kipolisi Tarime na Rorya, SACP Justus Kamugisha, alisema jeshi la polisi
linamshikilia mtu mmoja anaeshukiwa kuhusika na mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment