Habari za Punde

Rais wa Comoro awasili nchini kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya mapinduzi

 Rais wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa DR. Ikililou Dhoinine akiwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar na Kupokea na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwa ajili ya kuhudhuria kilele cha maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa DR. Ikililou Dhoinine  kwenye chumba cha watu mashuhuri { VIP }  hapo uwanja wa ndege wa Zanzibar.


Rais wa Jamhuri ya Comoro Mheshimiwa Dr. Ikililou Dhoinine akisalimiana na baadhi ya wana jumuiya ya Wakfi ya Wangazija hapa Zanzibar waliofika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar Kumpokea.

Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis Ame, OMPR

Rais wa Jamuhuri ya Visiwa vya Comoro Mheshimiwa Dr. Ikililou  Dhoinine amewasili Zanzibar leo jioni kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Kilele cha maadhimisho hayo kitafanyika katika uwanja wa amani Mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, viongozi wa kiserikali, siasa pamoja na wageni waalika kutoka baadhi ya nchi za kiafrika na zile rafiki.


Kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Mheshimiwa Dr. Ikililou alipokewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadhimisho ya Kitaifa Balozi Seif Ali Iddi.

 Balozi Seif pia aliambatana na Baadhi ya Mawaziri, makamanda wa Vikosi vya aUlinzi na usalama Nchini pamoja na Wanajumiya ya Wakfi ya Wangazia hapa Zanzibar wakiongozwa  Rais wao Profesa  Saleh Idriss Ahmed.

Mara baada ya kuwasi Rais huyo wa Jamuhuri ya Comoro na mwenyeji wake Balozi Seif waliangaliwa kikundi cha ngoma za asili kilichotayarishwa rasmi kwa ajili yake.

Jamuhuri ya Comoro imekuwa na uhusian wa muda mrefu na Zanzibar na Tanzania kwa ujumla hasa kutokana na wananchi wake kuingiliana kidamu jambo ambalo linafanya  watu wa pande hizo mbili wawe kama ndugu wa familia moja.

Mheshimiwa Dr. Ikililou Dhoinine anatarajiwa kurejea nyumbani Comoro kesho jioni mara baada ya sherehe za maadhimisho hayo ya miaka 50 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.
No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.